Wednesday, February 20, 2013

WASTARA NA MAMA SAJUKI WAANZA KUKWARUZANA...SOMA ZAIDI HAPA

IKIWA ni takribani siku siku 47 tangu alipofariki staa wa filamu za Kibongo, Juma Kilowoko ‘Sajuki’, kuna madai kuwa tayari visa vimeanza kati ya mkewe Wastara Juma na mama yake mzazi yaani mkwewe

 
Wastara Juma.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mama Sajuki amekuwa akidaiwa kumfuatilia Wastara kwa kila anachokifanya hadi kufikia hatua ya kuwaambia watu wamchunguze.
Chanzo hicho kilidai kuwa Wastara na mama Sajuki walifikia hatua ya kurushiana maneno mbele za watu huku ulemavu wa mjane huyo wa Sajuki ukitajwatajwa.
“Unaambiwa wakija watu kumuombea dua Wastara na kumwambia atapata mwanaume mwingine, mama Sajuki anashindwa kuvumilia na kujikuta akiangua kilio,” kilidai chanzo hicho.

Mama mzazi wa Sajuki.
Kiliendelea kudai kuwa siku moja Wastara alitembelewa na watu kwenye ofisi yake iliyopo ndani ya nyumba anayoishi, Tabata-Bima, Dar ambapo mama Sajuki alidaiwa kuwafuatilia watu hao akitaka kujua mazungumzo waliyokuwa wakifanya na mkwewe huyo.
Kiliendelea kutiririsha madai kuwa siku ya arobaini ya Sajuki, mama Sajuki aliwaka mbele ya kadamnasi akikasirishwa na kitendo cha Wastara kupiga picha akidai huko ni kujitangaza.
HUYU HAPA WASTARA
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa sakata hilo lilihamishiwa usiku kwani Wastara naye alikuja juu akiomba waweke kikao ili kuweka mambo sawa mbele ya baba Sajuki, mzee Juma Kilowoko.
Baada ya kujazwa habari hizo, dawati letu lilimtafuta Wastara ili kusikia upande wake juu ya ishu hiyo ambapo alisema kuwa pamoja na yote, kwa upande wake anamheshimu mama mkwe wake.
MAMA SAJUKI ALIKUWA NA HAYA
Alipotafutwa mama, alikuwa na haya ya kusema:
“Ni kweli nilipata uchungu sana wakati wa arobaini kwani mama aliyekuwa akiendesha dua (Mariam Dedesi), alikuwa akisema tumuombee Wastara apate mwanaume mwingine, kama mzazi ni kweli nililia kwa uchungu na kutamka maneno mazito,” alisema mama Sajuki.

No comments:

Post a Comment