Monday, February 11, 2013

WEMA SEPETU AIKARIBIA NDOAMuigizaji wema sepetu amejikuta akiwaweka watu roho juu mara baada ya meneja wake  mzee wa single Button Martin kadinda kuweka picha hii katika mtandao na kuandiaka kichwa cha habari "Usiniulizeeeeee" Watu walijikuta wakishindwa kujua nini haswa maana halisi ya picha hii na kuanza kuulizana kama ni kweli wema atakuwa kaposwa au lah!!

 Maswali mengi yalizuka kwani Wema alionekana  Kama mwanamke wa kiislam anayeenda kuolewa au kutolewa mahari. swali linakuja je anayemuoa ni nani? hadi sasa wema hajazunguza lolote japo hii majuzi alionekana katika picha na kibopa mmoja akiliwa mate katika picha na kufanya watu wahoji kama ndiye mwanaume anayetaka kumuowa au lah!!

Baadhi ya watu waliotowa maoni yao wamesema kuwa wema mtulivu alikuwa ni yule wema wa mr bluu na kanumba ila wema wa sasa hawamuelewi kwani anabadili wanaume kama nguo alisema jamila wa kawe huku anselemu wa chato yeye alisema anaamini wema ni mtu mzima na anajua anachokifanya hivyo haoni sababu ya watu kumjadili bora wamuache ajiachie tu,kwa upande wa mariamu yeye alisema anadhani wema kadata zaidi baada ya kuachana na Diamond.

Wewe unasemaje Mdau

1 comment: