Sunday, March 31, 2013

DIAMOND APOKELEWA KAMA MFALME HUKO BUKOBA, POLISI WAFUNGA BARABARA KADHAA.

Kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wasanii wa Tanzania wanavyozidi kukubalika kikazi hapa hapa nchini tofauti na miaka ya nyuma watanzania walionekana kuwashobokea sana mastaa wa nje lakini kwa sasa wanaokuja nchini  mapokezi yao huwa ya kwaida tu au hakuna mtu anayejali. 


Diamond anadhihirisha kuwa watanzania kwa sasa wanathamini wasanii wao kwa kitendo cha yeye kupokelewa kama mfalme jana huko Bukoba, kagera alipokwenda kufanya show. Mashabiki walijitokeza kwa wingi kumpokea kiasi cha polisi kulazimika kufunga baadhi ya barabara ili kuwe na hali ya usalama zaidi na pia mwanamuziki huyo apite kwa amani. Hii pia ni salamu kwa waandaaji wa matamasha ya muziki hapa nchini waliojawa na kasumba za ukoloni mambo leo na unyonyaji kwa kuwalipa mamilioni ya shilingi wasanii wa nje wakiwemo wa marekani hata kama hawana jipya huku wakiwalipa kinyonyaji wasanii wa ndani ambao wanakubalika sana tu. Pia hii iwe salamu kwa serikali kuthamini sanaa zetu kwa kuziba minya ya unyonyaji wa kazi zao. Angalia picha hizoooooooo............

No comments:

Post a Comment