Wednesday, March 06, 2013

HAWA NI WACHEZAJI WATANO WENYE UMRI ZAIDI YA MIAKA 40 LAKINI BADO WAMEENDELEA NA SOKA, YUKO ANAETAJWA KUWAFATA

.
Ronaldo.
1. Rivaldo – Kiungo wa zamani wa Barcelona, Ac Milan na timu ya taifa ya Brazil kwa sasa anaichezea timu ya Sao Caetano inayoshiriki ligi daraja la pili, alishawahi pia kucheza kwenye club ya Kabuscorp aliyoifungia magoli 11 kwenye mechi 21.
.
David James.
2. David James – ni kipa wa zamani wa England na Liverpool na kwa sasa anaichezea Bournemouth ya ligi daraja la kwanza England akiwa na umri wa miaka 42.
.
Schwarzer.
3. Mark Schwarzer ni kipa wa Australia anaeichezea Fulham, watu wengi wanausahau umri wake wanapomuona uwanjani na hii inatokana na wepesi wake golini.
.
Maldini.
4. Paulo Maldini (44) – ni beki wa zamani wa AC Milan na timu ya Taifa ya Italia, alicheza mechi zaidi ya 900 akiwa na Milan na mechi 126 akiwa na timu ya taifa, amewahi kutwaa Mataji matano ya ligi ya mabingwa, saba ya Seria A na alistaafu akiwa na umri wa miaka 41 na jezi yake namba 3 ikastaafishwa kwa heshima yake.
.
Derek.
5. Derek May ameripotiwa kuwa mchezaji mwenye umri mkubwa lakini anaecheza mpira kwa kiwango cha juu kabisa, umri wake ni miaka 74 ambapo amecheza kwenye mechi zaidi ya elfu mbili huku akifunga magoli zaidi ya 1300.

.
.
Kutokana na ukali alionao bado, mchezaji Didier Drogba ametajwa kwamba nafasi yake kwenye list ya wachezaji walioendelea kucheza soka baada ya kufikisha umri wa miaka 40 iko wazi, hiyo ni kutokana na ubora alionao sasa hivi japo umri wake ni miaka 34, anaingiza miaka 35 march 11 2013 siku tano zijazo.
.
Didier.

No comments:

Post a Comment