Wednesday, March 06, 2013

JB AUKUBALI UWEZO WA RAY NA KANUMBA ASEMA WAMEFANYA KAZI KUBWA KUFIKISHA FILAMU ZETU HAPA..AMPONGEZA MTITU GAME KWAKU WAWEZESHA

Msanii mkongwe ndani ya tasinia ya filamu nchini tanzania Jacob stephan jb au bonge la bwana amefunguka na kutoa ya moyoni na mwake na kuweka wazi kuwa kanumba na ray wamejitaidi sana kuifikisha sanaa yetu hapa ilipo leo.

Akipiga stori na dawati letu jb amesema yeye sio mchoyo wa fadhila na anaheshimu sana uwepo wa ray na marehemu kanumba kwani walifanya kazi kubwa sana tena ya maumivu,ya dhuluma,ya kudhalilika na kutukanwa hadi kuifikisha sanaa yetu hapa ilipo,akifafanua jb amesema ana amini kabla ya ray na kanumba walikuwepo wasanii wengi sana tena wazuri na hata yeye alikuwepo kabla ya ray na kanumba enzi hizo,Ila hawakufanikiwa kuwateka watu kama ilivyokuja kwa ray na kanumba, japokuwa tulikuwepo lakini kwa hekma za mwenyezi mungu aliwaleta vijana hawa katika sana na kufanya mabadiliko makubwa hadi kufikia filamu zetu kuitwa filamu za ray na kanumba kwa nchi za jirani.

Jb alifika mbali zaidi na kusema Hawa vijana ya watu ninaowaheshimu sana kiukweli mtu akiwadharau haijui tulipotoka,mimi sina maana kwamba sisi tuliobai sio wazuri hapana ila hata katika timu wote wanaumuhimu ila mfungaji ni mmoja goli halifungwi na watu wawili japo husababishwa na wengi hadi mfungaji kufunga.

JB aliendelea kumueelezea  kanumba kama shujaa asiyeogopa na ambaye alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha tanzania tunafikia levo za kimataifa zaidi Nadhani mtakubaliana na mimi kuwa kanumba alikuwa ni upepo kwa wasanii wa tanzania kwani kila alipovuma na sisi tulifuata ili mradi tufike alipo yeye mtakumbuka pia alituunganisha na wasanii wa kimataifa na kufanya tuamini kama mungu angempa uzima basi leo pengine tungeshashiriki movie na watu wa hollwood kutokana na juhudi za haraka alizokuwa anazionyesha ndugu yetu.

JB amemuelezea ray kama mtu ambaye haogopi na akiamua kufanya kitu huwa hajali nani kasema wala itakuwaje ndio maana hadi leo ray anakuwa ni msanii anayeongoza kwa wasanii wenye vifaa vingi na bora vya utengenezaji wa filamu tanzania huku akiendelea kuongoza kwa utengezaji wa picha zenye kiwango kizuri na kikubwa sana tofauti na movie nyingine ambazo hadi leo bado ni tatizo kwenye sauti na picha ila kwa ray hilo amefanikiwa tena kwa levo za juu kabisa.

Jb amesema anawashangaa sana watu wanaosema ray hauzi amesema waache kuchukua maneno ya chini ya mbuyu na badala yake yeye anakiri kuwa ray anauza sana kuliko maelezo na movie zake zinaongoza kununuliwa kwasababu zinaongoza kwa kwaliti na anajua kuziongoza vyema ndio maana hata soko la ndani na nnje amelishika.

Pia jb alimshukuru mtitu game na kumita ni mkombozi na mleta mabadiliko ya sanaa ya tanzania.jb ni kati ya mastaa wanaotajwa kumiliki mkwanja mrefu sana kwa sasa na pia ana mashabiki wengi sana kwa sasa.  

No comments:

Post a Comment