Monday, March 25, 2013

LUCY KOMBA NA TOX STAR MAMBO HADHARANI..LUCY AELEZA KILA KITU..FILAMU YAKE YA DAR TO DENMARK MBIO KUTOKA


Msanii lucy komba

Msanii wa filamu nchini tanzania ambae ameshavuka mipaka na kufanikiwa kufanya filamu nchini ghana,Brundi,Seralion na denmark mwanadada lusi komba amefunguka na kuiongelea filamu yake mpya anayotarajia kuiachia hivi karibuni iitwayo tanzania to denmark ambayo amewashirikisha Slimu omary,Toxt star na yeye mwenyewe kwa upande wa tanzania huku wasanii wengine wakitokea huko huko denmark.

Msanii lucy komba akiwa nchi Denmark
Akiongea na thesuperstarstz mwanadada huyo mkali wa movie amesema ,Ni kweli nimefanya filamu kote huko na sasa ninampango wa kuiachia filamu yangu mpya inaitwa tanzania to denmark na ninaahidi mengi kwa watanzania katika filamu hiyo kwani ni filamu iliyoshutiwa tanzania na denmark.

Lusi ameweka wazi kuwa kwasasa hatakubali kurudi nyuma tena na anachokitegemea zaidi ni maombi ya watanzania na wadau wa filamu popote walipo.thesupestarstz ilipomaliza ilimuuliza mwadada huyo kuhusu skendo iliyoinyaka chini ya kapeti juu ya mahusiano yake na Msanii mwenzie ambaye ni mwanamuziki wa bongo fleva toxt star aliyewika sana na ngoma yake ya prety garl aliyomshirikisha Ally kiba.

Msanii anayedaiwa kuwa ndiye mpenzi wa lucy komba kwa sasa Tox star
Baada ya thesuperstarstz kumsomea msanii huyo mashtaka yake mwanadada huyo alijikuta anacheka na kusema.Haa haha haaa We nani kakuambia habari hiyo jamani?mimi na toxt ni marafiki tu na pia ni msanii mwenzangu sasa siwezi kuwazuiya watu kusema juu ya habari hiyo ila soon watajua kama kweli au si kweli alisema msanii huyo ambaye hata ukimuudhi yeye ni mtu wa kutabasamu tu muda wote thesuperstarstz baada ya kuongea na lusi ni kama haikuridhika na sana iliamua kumsaka toxt star ilikujua na kulinganisha habari hiyo ambapo toxt alisema Unajua kaka kila lisemwalo lipo na kifupi siwezi kuifunga midomo ya watu maana hili jambo lilianza kama mzaha sasa na shangaa nyie mmeipata wapi habari hii.

Msanii lucy komba katika pozi
Kauli hiyo ilimchanganya sana mwandishi wetu na kutaka kujua zaidi habari hii ndipo ilipomtaka msanii huyu wa bongo fleva kujiweka wazi juu ya habari hii kama ni kweli au si kweli Kaka narudia tena lusi ana maisha yake na mimi na maisha yangu alafu lusi ni mwanamke na mimi ni mwanaume sasa kuna shida gani kama akiwa mpenzi wangu?Alisema msanii huyu mkamata maiki stejini na kukata simu.


Hapa msanii lucy komba akiwa na wasanii wenzake huko Denmark

Tulifanikiwa pia kuongea na watu wa karibu sana na msanii lusi ambao waliomba kuhifandhiwa majina yao wa kwanza alisema Mbona hizi habari zipo wazi sema wanaogopa tu magazeti ila hakuna la kujificha hapo hawa ni wapenzi na kama hamuamini mtajua muda si mrefu mapenzi hayajifichi bwana kilisema chanzo hicho cha habari hii.


Msanii Tox star katika pozi

Hadi tunaenda mitamboni kuiandika habari wawili hao walikuwa wanakanusha habari hiyo ila tunakuahidi mdau kuwa tutawafuatilia na tutakapojua ukweli tutawaletea hapa hapa kwani thesuperstarstz ndio chanzo cha habari za mastar

No comments:

Post a Comment