Friday, March 08, 2013

MASTAA WA FILAMU RAY,JB,UWOYA,NA KING MAJUTO WANATARAJIWA KUTUA KIGALI RWANDA KWA MUALIKO MAALUMU

Mwenyekiti wa bongo movie Vicent kigosi (Ray) katika pozi

Wale mastaa wa filamu nnchini tanzania Vicent kigosi Ray,Jacob Stephan Jb,Irene uwoya,na yule king wa vichekesho nchini King Majuto kwa pamoja wanatarajiwa kutua nchini rwanda kwa mualiko rasmi uliowataka kwenda nchini humo.

Wasanii hao wamepata mualiko huo kutokana na nchi hiyo kuzikubali sana kazi za wasanii watanzania na kuona njia pekee ni kuwaita  kwaajili ya kuwapa nguvu wasanii wao,Akizungumza na thesuperstarstz huko kigali kwa njia ya simu Ndwimana Ngikonwa ambaye ni mmoja wa mapromota wa nchi hiyo amesema yeye anawafahamu sana wasanii hao na amefurahishwa sana na ujio wao kwani itasaidia kuleta changamoto kwa wasanii wao.

King Majuto atakuwepo
Jacob stephan Jb atakuwepo pia
Promota huyo ambaye inasemekana alishawahi kuwachukua wanamuziki kibao toka bongo kwenda kupiga shoo huko kigali anaendelea kusema kuwa kama wasanii hao watakubaliana nae atawapa dili jingine mara baada yakumaliza kazi iliyowapeleka, Tulipomuuliza kama anahusika na safari hiyo alikana nakusema hapana ila anajua mchongo wote na kuendelea kusema kuwa hakujiingiza kwenye inshu hiyo kwani imekaa ki serekali zaidi bila kufafanua maana yake.

Uwoya na Jb katka pozi wakati wakirekodi filamu
The superstarstz ilipomalizana na promota huyo ilimuendea hewani Jb kama mmoja wasanii waliotajwa katika safari hiyo  kutaka kujua ukweli wa habari hizi na alipopatikana alisema,Ni kweli kaka tunasafari ya huko ila mengi mpigie Ray kwasababu yeye ni mwenyekiti wa bongo movie atakueleza mengi zaidi kama kiongozi wetu   

The superstarstz ilitaka kujua kama safari yenyewe ni kweli inahusu mwaliko wa serekali ambapo Jb alijibu kwa kifupi yote mtajulishwa na ray, 


Ray na Uwoya katika  picha za filamu ya PRETTY GIRL
Tulipomalizana na jb moja kwa moja thesuperstarstz ilimuendea hewani msanii Vicent kigosi ambae ni mwenyekiti wa bongo movie kwa sasa na kumuuliza kama yeye na vijana wake wana safari ya kigali nchini Rwanda. Nae kama jb alikiri kuwana na safari hiyo na hapo ndipo thesuperstars ilipotaka kujua kinachowapeleka rwanda ambapo ray alisema Ni safari ya kawaida kaka unajua kwa sasa tunamshukuru mungu sana kwani imefika hatua nchi jiran wanaamini sisi tunaweza kuwa chachu ya wasanii wao kufanya vizuri katika filamu na hili limefanya tuitwe huko.

Tulipotaka kujua kama safari hii inahusisha serekali ray alicheka na kusema Unajua wenzetu ni tofauti na sisi wao kila kitu kinaenda kisheria huwezi kufanya jambo mpaka chama kijue na kikishajua ni serekali japo sisi kama sisi tutakutana viongozi mbali mbali wa nchi hiyo kwa sababu nnchi nzima ya rwanda imeshajua na imejiandaa kwa ajili yetu na imeandaa mapokezi makubwa sana wanasema wanataka yavunje yazidi yale ya congo niliyoyafanya nikiwa na swahiba marehemu steven kanumba.
Uwoya katika pozi
Ray alipoulizwa wataondoka lini kuelekea huko amesema kesho nitakupa jibu kaka maana mambo yote yapo poa ila elewa muda wowote kuanzia leo tutaondoka Nae kiongozi wa msafara amesema kuwa katika ziara hiyo wasanii hao wanatarajia kukutana na mheshimiwa raisi na kumuelezea kiundani wigo wa sanaa na nini kifanyike kuinua sanaa ya rwanda Ray amewataja wasani atakao ongozana nao kuwa ni pamoja na Irene uwoya ,,Jacob Stephen Jb, na Mzee King Majuto the superstarstz inawatakia kila la kheri na kuwaomba waitangaze tanzania kila dakika watakayopata nafasi hiyo.

2 comments:

  1. hongereni sana na karibuni rwanda

    ReplyDelete
  2. HAKIKISHENI HATUANGUSHI

    ReplyDelete