Wednesday, March 06, 2013

MATUMAINI AIANGUKIA SERIKALI IMSAIDIE MATIBABU YA INI NA FIGOKOMEDIANI maarufu Bongo, Tumaini Mwakibibi ‘Matumaini’ ameiomba serikali imsaidie kupata matibabu ili aweze kupona maradhi ya figo na ini yanayomkabili.

Akizungumza na mwandishi wetu jijini Dar es Salaam alisema: “Hali yangu bado si nzuri ingawa natumia dawa lakini sijapata tiba sawasawa. Sina fedha na familia yangu kwa sasa imeishiwa kwa sababu magonjwa yanayonisumbua ni makubwa na yanahitaji fedha nyingi.

“Naiomba serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo isikie kilio changu. Hali yangu si nzuri, nahitaji msaada ili kuokoa maisha yangu. Nina imani  nikipata tiba kamili nitapona na kurejea tena jukwaani.

No comments:

Post a Comment