Thursday, March 07, 2013

MBUNGE SHAROBARO WA KENYA AMSHINDA MPINZANI WAKE KWA KURA ZAIDI YA LAKI NANE

..
.
Pamoja na Usharobaro wake, Gideon Mbuvi maarufu kama Sonko… yule mbunge aliependwa na wengi na anaejichanganya sana na watu wa kipato cha chini ametangazwa mshindi wa kiti cha Useneta wa Jiji la Nairobi Kenya ambapo alitoa machozi kwa kutoamini kama kweli ameshinda.
Hiyo picha hapo chini japo haionekani vizuri inamuonyesha Sonko wakati akitangazwa mshindi, alikua kapiga T shirt yake ya njano, kofia na hereni pia kama kawaida… alafu kwenye mkono akatupia pete kadhaa za gold pamoja na saa kubwa mkono wa kushoto.
.Sonko ambae amepata umaarufu kwa Usharobaro wake pia ambao ulimfanya kuwa Mbunge wa kwanza kwenye historia ya Kenya kuingia bungeni amevaa hereni, ameshinda kwa kupata kura zaidi ya laki nane wakati mpinzani wake Wanjiru aliepata kura laki tano.
Sonko ni mtu wa kujichanganya sana, nakumbuka hata wakati ule Z Anto wa Binti kiziwi yuko juu kwenye chati, Sonko alimpatia usafiri pamoja na walinzi wa kutembea nae wakati alipoalikwa kwenye kupafom Kenya.

Kifupi mbunge huyu ni taa na nyota ya vijana kwani anapendwa sana na pia yeye anawapenda vijana na anawasaidia sana hasa wale walio na maisha magumu amekuwa kimbilio,The supestars tz iliongea na baadha ya wasanii na vijana wa kenya wote walikiri kuwa hakuna mbunge mwenye macho ya kuona wenye shida kama sonko kwani si mara moja ametowa misaada kwa vijana hivyo ushindi kwake ulitegemewa kwa asimia kubwa.

Mbunge huyo sharobaro amewaeleza waandishi wa the super stars tz ambao wapo nchini kenya kufuatilia zoezi hili la uchguzi kuwa ameupokea ushindi huo kwa furaha na amewa ahidi wakenya kushirikiana nao kwa shida na raha kama awali huku aki ahidi kuwafanya vijana waipende nnchi yao kwakuwapa fursa kibao zitakazo wafanya wapate kipato kizuri,sonko ameendelea kusema imani yake mungu alitaka kila mtu aishi maisha mazuri yaani kusiwe na maskini wala tajiri ila ana imani wanadamu ndio tumebadili mfumo huo kwa tamaa zetu hivyo atahakikisha nguvu ya kijana haipotei inatumika kwaajili ya kuingiza pesa.No comments:

Post a Comment