Saturday, March 09, 2013


Mwana FA akanusha kuwa na mipango ya kugombea ubunge mwaka 2015


Rapper Hamis Mwinjuma aka Mwana FA amekanusha tetesi kuwa ana mpango wa kugombea ubunge katika moja ya majimbo ya mkoani Tanga anakotokea na kudai kuwa lengo lake ni kuisaidia jamii lakini si kwa kupitia siasa.
MWANAFA-NEW
Akiongea na 255 ya Clouds FM, Mwana FA amesema kwa nafasi aliyonayo kama msanii anaweza kuisaidia jamii bila ya kuwa mwakilishi wa kisiasa.
“Kusaidia jamii sio lazima uwe mwanasiasa sababu kuna watu kibao wanaofanya kama wanaharakati tu, ukasaidia ambapo kuna matatizo, kuna watu wanaweza kupandisha sauti zao wakawafanya watu wawe aware na matatizo ambayo labda walikuwa hawajayasikia na wana namna ya kuyatatua wayatatue,” alisema FA.

No comments:

Post a Comment