Saturday, March 16, 2013

RAY, KING MAJUTO, JB NA IRENE UWOYA WATIKISA RWANDA

.Irene Uwoya

Irene Uwoya mwigizaji wa filamu Sawhiliwood.
WASANII nguli katika tasnia ya filamu Swahiliwood Ray, JB, King Majuto na Irene Uwoya walikuwa gumzo katika tamasha la utoaji tuzo nchi Rwanda ambapo msanii kama Irene Uwoya ilibidi jina lake la asili lipotee na kujikuta akikumbushwa enzi za nyuma alivyotesa katika filamu iliyotamba na kuwa gumzo ya Oprah on Sunday.

.
Jacob Stephen, Vincent Kigosi
JB akiteta jambo na Ray .
vincent Kigosi
Ray akifuatilia utoaji wa tuzo za Rwanda Movie Awards.
Vincent Kigosi, Irene Uwoya, Athuman Amri
King Majuto kwa nyuma na Ray , Irene Uwoya wakifuatilia kwa makini utoaji wa tuzo.
Irene Uwoya
Irene Uwoya akifuatilia Rwanda Movie Awards kwa makini.
Matangazo katika redio televisheni jina lilokuwa likisikika ni Oprah umugore wa Katawuti wakimananisha kuwa Irene mke wa mchezaji wa mpira Ndikumana, jina la Oprah limekuwa ni jina maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha wasanii nyota marehemu Steven Kanumba na Vincent Kigosi ‘Ray’.
Wanyarwanda walilipuka ukumbi huku wakiita Oprah na Ray wakimwita Kigozi badala ya Kigosi, tuzo hizo zilizopewa jina la Rwanda Movie Awards zikilenga kuwatunuku wasanii wa filamu wa nchi hiyo na wasanii kutoka Bongo wakiwa kama watu mashuhuri waliofika kutoa zawadi kwa washindi walichaguliwa Rwanda Movie Awards.
Tamasha hilo la utoaji wa tuzo liliandaliwa na Ishusho Arts na kutoa mwaliko kwa nyota wa filamu kutoka Swahiliwood, pia wasanii hawa waliweza kuona na viongozi wa nchi hiyo na kubadilishana mawazo kama wageni wanaowakilisha wasanii Afrika Mashariki.

Baada ya kutua hapa nchini the super stars tz iliwapokea wasanii hawa na kutaka kujua hali ya kule rwanda ambapo ray alisema anawashukuru wanyarwanda kwa mapokezi makubwa kwa upande wa mzee majuto alisema amefurahi sana kwa waandaji kuona anafaa kuwa mmoja kati ya wasanii waliochaguliwa kutowa tuzo naye jb alisema kuwa kwenda kwao rwanda ni kuliwakilisha taifa lote la tanzania hivyo anaamini wametenda haki kama wadau wa tanzania walivyowaagiza,kwa upande wa uwoya ambaye kwake alikuwa na kazi mbili kwanza kuliwakilisha taifa pili kuwa ukweni.

No comments:

Post a Comment