Monday, March 11, 2013

RAY,JB,UWOYA,NA KING MAJUTO WAPATA MAPOKEZI YA NGUVU NCHINI RWANDA


Msanii vicent kigosi (Ray)

wasanii ray,jb,uwoya na king majuto ambao walikuwa safarini huko nchini rwanda wameongea na thesuperstarstz wakiwa huko nchini rwanda na kueleza kufurahishwa kwao na ziara yao na kuwashukuru wanyarwanda kwa mapokezi makubwa ambayo binafsi hawakuyategemea.
Msanii Jacob stephan (Jb)

Akizungumza na sisi kwa njia ya simu kiongozi wa bongo movie Vicent kigosi Ray Amesema kuwa binafsi amefurahishwa na mapokezi ya wanyarwanda na kuongeza kuwa ni watu wa karimu sana na ameahidi kushirikiana nao kila watakapo muhitaji kwani amegundua vipaji vingi nchini humo.


Msanii Irene Uwoya


Msanii King majuto
Kwa upande wa msanii Jacobu stephasn au Jb Amesema katika maisha yake aliamini watu wa rwanda ni wakorofi na bado vita inaendelea lakini ameshangazwa na mapokezi waliyoyapata na utulivu uliopo nchini rwanda.


Wasanii hao ambao walipata mualiko rasmi nchini humo wamemaliza ziara yao na sasa wapo njiani kurejea nchi kwa mujibu wa kiongozi wa msafara huo.

No comments:

Post a Comment