Saturday, March 09, 2013

SAMAHANI KWA PICHA HIZI ANGALIA  MWANAMKE HUYU ALIYEOKOTWA AKIWA AMEKUFA HAPA MOROGORO

WANANCHI WAOMBWA KWENDA  KUANGALIA MAITI YA MWANAMKE  HUYO

Maiti ya Mwanamke imeokotwa kwenye mashamba ya mkonge Mkoani morogoro.Taarifa zaidi zinasema mwili huo uliokotwa machi 2 mwaka huu katika mashamba hayo ya mkonge  alikutwa amenyongwa kwa kutumia nguo.
Jeshi la polisi wameomba wananchi wa mkoani hapa kufika katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kuangalia mwili wa mwanamke huyo ambaye bado hajafahamika na ambaye aliuawa kisha mwili wake kutelekezwa kwenye mashamba ya mikonge nje kidogo ya mji Morogoro.


Taarifa zaidi zinasema kuwa baada ya polisi kufika katika eneo la tukio na kuukagua mwili huo waligundua sehemu ya shingoni mwanamke huyo alikuwa na majeraha,,, thesuperstarstz ina muomba mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi amin

No comments:

Post a Comment