Friday, March 29, 2013

TAMASHA LA KUMKUMBUKA KANUMBA LANUKIA...ANGALI KILICHOFANYA WATU WASEME KANUMBA KAJITABIRIA KIFO CHAKE

Marehemu steven kanumba enzi za uhai wake akiwa katika moja ya scen za love and power ambayo ni filamu yake ya mwisho

Zikiwa zimesalia siku chache  kufika April,7 siku ya kukumbuka kifo cha Marehem Steven Kanumba,ambapo atakua akitimiza mwaka mmoja tangu atutoke hapa Duniani wasanii na wadau mbali mbali wamejipanga kufanya tamasha kubwa na la bure ili kumuenzi msanii huyo aliyepigana kuifikisha na kuitangaa vyema sanaa ya tanzania ndani na nnje ya tanzania.

Katika kumuenzi Marehemu litafanyika tamasha kubwa na la bure kabisa pale Leaders Club, Watu kutoka sehemu mbali mbali za tanzania watakutana pale kwa lengo la kumuenzi na kuangalia yale aliyofanya enzi za uhai wake ikiwa ni pamoja na kuzindua Filamu yake ya mwisho itwayo "LOVE AND POWER"  
   

Hapa wakiwa katika scen kabla ya kugombana
Raisi wa shirikisho la filamu nchi bwana Saimoni mwakifwamba ameongea na thesupestarst mapema hii leo na kueleza kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika na anamini wadau na watanzania kwa ujumla watajitokea kwa wingi kumuenzi msanii huyo huku akisisitiza kuwa ni bure kabisa .

Kwa upande wa Seth bosco ambae ni mdogo wa marehemu amesema kuwa tamasha hilo limeandaliwa mahususi ili kuendelea kumuenzi marehemu na pia kuleta changamoto kwa wasanii wengine kuiga mfano wa kanumba ili kuinua sanaa ya tanania.
 
Nnje ya kumbukumbu hiyo pia katika tamasha hilo wataizindua filamu ya mwisho kabisa kwa maremu kanumba itwayo LOVE AND POWER nadhani tunakumbuka kuwa filamu hiyo ndiyo filamu iliyofananishwa matukio na kifo cha nguli huyo wa filamu nchini.

Hii ndio scen  Irene poul aliyomsukuma kanuma japo hakufa na wala hakupata madhara kifilamu nayo ipo ndani ya filamu yenyewe
Watu wengi wamejaribu kuifananisha filamu hiyo na kifo cha kanumbaleo kwa ufupi ngoja niwaletee mambo ambyo yapo ndani ya filamu na baadhi ya matukio ya kifo chake
Ni kweli msanii irene poul alimsukuma kanumba ila hakufa wala hakujigonga japo inafanana na tukio lililomkuta hadi kupotea maisha 2 docta unayemuona hapo katika picha ndio docta wa kweli wa msanii huyo na ndiye aliyefika baada ya kumbiwa kanumba kaanguka kiukweli nnje ya filamu japo katika filamu hakucheza kama docta wake alikuwa docta wa kawaida tu.3 Hali ya kusukumwa na kitanda ilikuwepo kweli ila kanumba hakufa na badala yake rafiki yake alijua kafa nakuanza kuchanganyikiwa ila scen inayofuata yupo hai,
 kiukweli ni filamu iliyofungana na matukio mengi na ndio maana hata watu wakaichukulia kama alitabiri kifo chake .
Huyo Doctor wa kiume unayemuona nnje ya filamu ndiye alikuwa doctor wa kanumba kabisa na hii scen ni wakati wa kumfanyia upasuaji ki filamu inapatikana pia katika filamu hiyo
Baadhi ya wasanii wameongea na the super stars tz nakuliongelea tamasha hilo kuwa ni tamasha kubwa na la kihistoria litakalokuwa linafanyika kila ifikapo April 7 ikiwa ni kumkumbuka marehemu ambae wamemtaja kama shujaa ambaye alikuwa haogopi kujaribu. pili ni msanii aliyepigania haki na maslahi kwa wote mfano muri ni wakati alipokuwa anapigania umoja wawasanii na kutaka tusaidiane na kusisitiza kama tuliungana tukamsaidia cloud 112 basi tuungane tena kumsaidia kajala ambaye nae yupo jela (japo nae katoka tiyari).walisema wasanii hao.
Hii ndio picha watu wanaosema alikufa katika mchezo hapa Marehemu kanumba akiwa katika scene hapa ni tukio la kusukumwa kama maiti baada ya kumaliza upasuaji kimchezo  lakini inapatikana katika filamu ya LOVE AND POWER
Baadhi ya wasanii hao ni pamoja na Vicent kigosi ray,jacob stephan jb,Iren uwoya,Jacklin wolper,Jenifa kyaka Odama,Shamsa ford,Single Mtambalike Rich Rich,Juma chikoka chopa Mahusen Awadhi Dk Chen,Wema sepetu,Blandina chagula Johari na wengine wengi ambao kwa pamoja wanaahidi kufanya yale yote mauri aliyoacha marehemu kanumba huku wakiwaomba watanzania waje kwa wingi kama tulivyomuaga msanii wetu huyo na sasa ni kumbukumbu kwetu kwakukuwa tulimpenda sana ndugu yetu Steven kanumba

2 comments:

  1. apumzike kwa amani AMINA

    ReplyDelete
  2. Atabaki kuwa jembe kwani ni wai amesaidia sana kuinua na kutangaza sanaa ya filamu na ndani na nnje mungu akupumishe kwa amani jembe

    ReplyDelete