Thursday, March 07, 2013

 TAFF WAMNG’OA KATIBU WAO BWANA MAKUBI.

Wilson Makubi
                      Katibu wa TAFF Wilson Makubi aliyetimuliwa na mkutano mkuu.

WAKATI Mkutano mkuu wa shirikisho la wasanii TAFF ukiendelea hali imekuwa mbaya kwa katibu wa shirikisho hilo Wilson Makubi baada ya kutimliwa na mkutano huu kwa sababu za ubadhilifu wa fedha za washindi wa mashindano ya muswada (Script) yaliyoandaliwa na shirikisho hilo na kupata udhamini wa PSI, habari za ndani zinasema kuwa katibu huyu bwana Wilson Makubi aliwakata washindi sehemu ya fedha hizo na kujimilikisha.

.
Simon Mwakifwamba
                                                   Rais wa TAFF Mwakifwamba

Tuliweza kuongea na Rais wa shirikisho hilo Simon Mwakifwamba na kukiri kuwa ni kweli Makubi amewajibishwa kutokana na kujitengenezea fedha kwa njia isiyo halali, Rais alisema kuwa baada ya kubaini baadhi ya makosa kamati kuu kwa mamlaka iliyo nayo ilimpiga chini bwana Makubi na nafasi yake kuchukuliwa na mwanaharakati wa siku nyingi katika tasnia ya filamu nchini Bishop Hiluka.
Ni kweli mkutano mkuu wa TAFF umemfukuza katibu aliyekuwepo madarakani Wilson Makubi, kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika fedha za washindi wa shindano la uandishi wa muswada (Script) baada ya kugundua kuwa fedha hizo hazikuwafikia walengwa kwa kiwango kilichopangwa, fedha ambazo zilikuwa ni kutoka PSI,”anasema Mwakifwamba.

Wilson Makubi
Katibu wa TAFF Wilson Makubi aliyetimuliwa na mkutano mkuu.

matokeo yalitoka na washindi kupatikana ambapo washindi walikuwa ni Chrissent Mhenga, Amri Bawji, Ignas Mkindi, Kauzeni John, na Kanuti hapo ndio sinema ilipoanza kwani washiriki walifika na kusainishwa kwa zawadi ya milioni moja, huku fedha zikiwa katika bahasha, awali waliambiwa kuwa watalipwa lakini nane kufuatia makato hayo.

Lakini katika mshangao mkubwa walijikuta wakiambulia laki sita baada ya kusaini kuwa wamelipwa milioni moja, the super stars tz ilijaribu kumtafuta kwa njia ya simu Wilson Makubi lakini hakupatikana.

Katibu mpya bwana Bishop Hiluka
Akizungumza na sisi katibu mpya wa TFF Ambaye ameanza kazi hii leo kwa mujibu wa raisi wa shirikisho la filamu bwana mwakifwamba katibu hiluka amesema anaiheshimu sana tasinia ya filamu nchini na ana ahidi kupambana sana kwa ajili ya maslah ya wasanii pia ameongeza kuwa ujuzi alioupata na unaotumiwa na mataifa mengine atajitaidi kuweka mezani ili kupiga hatua kwani lengo nikuifanya sanaa ya tanzania kuwa ya kipekee na ya kusifiki kwa maslahi ya msanii na taifa kwa ujumla.

3 comments:

  1. Huu ubabaishaji hadi lini jamani tutafika kweli

    ReplyDelete
  2. kaka we acha tu bado ni kitendawili

    ReplyDelete
  3. Watu hawana hata huruma wanatafuna hadi pesa ya msiba sasa hiyo wataiacha vipi

    ReplyDelete