Saturday, March 16, 2013

WANYARWANDA WAIKOMALIA NDOA YA IRENE UWOYA,


KATIKA kile kilichoonekana ni kuikomalia ndoa ya msanii wa filamu Bongo Irene Uwoya, baadhi ya wadau nchini Rwanda wameendelea kutambua kuwa yeye ni mke halali wa msakata kabumbu, Hamad Ndikumana ‘Kataut’.

Hayo yalibainika hivi karibuni baada ya Uwoya, Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Jacob ‘JB’ na Amri Athuman ‘King Majuto’ kutua nchini humo kuhudhuria utoaji wa tuzo za filamu zilizopewa jina la Rwanda Movies Awards.
Wakiwa Rwanda, matangazo yaliyokuwa yakirushwa kupitia redio na televisheni yaliainisha kuwa Uwoya ni mke wa Ndikumana, kitendo kilichowashangaza wasanii hao.

Akizungumza na THESUPERSTASTZ hivi karibuni, mmoja wa wasanii aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema, inavyoonekana Wanyarwanda wengi hawataki kuamini kuwa ndoa ya Uwoya na Ndiku haipo na ndiyo maana wameikomalia.
“Katika matangazo yaliyokuwa yakisikika katika redio na televisheni, jina lililokuwa linatajwa ni Oprah umugore wa Kataut, wakimaanisha Oprah mke wa Kataut.
“Jina la Oprah kwa Uwoya limekuwa maarufu nchini Rwanda kufuatia filamu ya Oprah on Sunday iliyowashirikisha yeye, Ray na marehemu Kanumba,” kilieleza chanzo hicho.

No comments:

Post a Comment