Friday, March 15, 2013

WASANII WA MOVIE NA MUZIKI WAUNGANA NA MASHABIKI KUMTETEA DIAMOND

Msanii Diamond plutnum
Msanii mkali na ambaye anaongoza kwa kuandikwa sana katika vyombo vya habari Diamond platnum ameanza kupata furaha mara baada ya mashabiki kuanza kumtetea na kuonyesha kukerwa na habari zinazoendelea kuvuma kila kukicha katika magazeti,redio na hata katika tv na blog mbali mbali kuwa yeye ni fremason na nyingine zikisema anategemea waganga.
 
Moja Show zake Uwanja wa Taifa

Kwa wiki kadhaa sasa thesuperstarstz imefanya utafiti  na kugundua jinsi msanii huyo anavyokubalika katika jamii na hata kwa wasanii wenzake.Nadhani  utakumbuka msanii Prof jay aliwahi kuandika akimtetea msanii huyu na kusema tuache majungu na kama dogo kakosea inafaa aitwe na arekebishwe na si kumponda na kumshusha kisanii kwa skendo,

Akipata picha na mashabiki wake
Hapa akipiga Kinanda Huku Anaimba
Hivi karibuni pia baadh ya wasanii katika page na twet zao wameonekana kuponda jinsi watu wanavyoibuka kwa kusema wao ndio waganga wanaomfanya msanii huyu kukua kisanii,wengine wakimsema mganga huyo kuwa kama anataka kumshusha Diamond basi ajipandishe yeye aimbe au awasaidie ndugu zake waimbe ili wapate pesa kama diamond na wasaidie.Wadau hao wamefika mbali na kulaani maneno ya watu kumzushia msanii huyo kuwa yeye ni fremason ...Kiukweli kwa sasa hapa nchin tanzania kumeibuka tabia ambayo hata haileweki imetokea nchi gani hadi kufika hapa kwani msanii akifanikiwa kidogo tu basi ujue atahusishwa na fremanson,nadhan mtakubaliana na mm kuwa hata kwa marehem kanumba walisema ni fremason wakaja kwa ray,jackline wolper na sasa kwa Diamond sasa swali la kujiuliza ni kwamba kuna mtu hata mmoja ambaye alikutana naye huko kwa hao jamaa akathibitisha juu ya uhalali wawasanii wetu kuwa huko?ukiwauliza utasiki sijakutana nae lakini huoni amepata mafanikio ya haraka lazima atakuwa fremason yule jaman hebu tubadilike tuswe watu wakumuabudu shetan kila saa alisema mama brayan

Kiukweli inakatisha tamaa na tutabaki hivi hivi hatutakuwa na wasanii wazuri wala wachezaji wazuri kwa sababu hatujui kuthamini vya kwetu alisema bwana mikidadi wa masaki huku bwana ally jo akisema anashangazwa sana na staili ya hapa bongo Nadhani hii inatokana na watu kuijua fremason juzi juzi ndio maana kila mtu akipata pesa kidogo tu za kununua nyanya basi ni fremason hebu tuelimike jaman tuache ubabaishaji tupende na kuthamini wasanii wetu 
Msanii Jackline Wolper

Baada ya yote hayo thesuperstastz ilimvutia waya jack wolper na kumuliza anajisikiaje kuhusishwa na iman ya fremason.Binafsi sipendi kuhusishwa na jambo ambalo sijalifanya wala sina ndoto nalo na siwezi kulifanya hebu jiulize super star mimi na fremason wapi na wapi kwa pesa gani nilizo nazo hadi niwe fremason hebu watu wasitake kujulikana kwa kutunga habari za uwongo,Utasikia eti diamond naye ni fremason jaman kwa hiyo prado au?basi hao fremason wana kazi.Alisema jack huku akionyesha dhahiri kukerwa na watu hao wanaotunga habari za uwongo
Msanii vicent Kigosi (Ray)

Kwa upande wa Ray alisema yeye hana la kusema kwani kama ni maneno kashayazoeya hivyo hawezi kumzuiya mtu kusema maana ni binadamu na wamezaliwa  wanasema kwa hiyo hawampi tabu.Unajua kaka hawa ni binadamu huwezi kuwazuiya cha msingi ni kufanya kazi sana ili uendeleze maisha yako ila ukiwasikiliza utaharibikiwa ndugu yangu,mimi nimezoea ila na mshauri mdogo wangu dimond akomae afunge masikio kwa yale anayoona hayana faida  na afungue masikio kwa yale  yenye faida na yeye Alisema ray Kwa upande wa Diamond alisema kuwa bado anaimani kubwa sana na mashabiki wake kuwa hawatamuangusha kwa kukuwa amekula kiapo kuwatumikia na kamwe hatafanya kinyume na hilo....Kaka sina mengi ila nachoweza kusema mashabiki wangu wasivunjike moyo haya ni mapito tu na yataisha so cha msingi wajue Diamond wao ni yule yule wa kamumbie mbagala ni yule yule wa kesho so nawapnda sana hizo ni stori tu kama movie na mungu atawanyoosha kwani yeye ndiye anayenijua zaidi yao kikubwa sintatetereka kwa maneno yao nimeandaa nyimbo za kutosha kwa ajili ya watu wangu u know sasa hayo maneno hayatani felisha kwakuwa namtegemea mungu.Alisema Diamond
Moja ya Show zake

Kwasasa Diamond ni msanii anayeongoza kwakufanya shoo nyingi sana ndani na nnje ya nchi huku wengine wakimtaja kama msanii mwenye mafanikio zaidi,kwa upande wake dimond amesema anashukuru mungu kwa kupiga hatua na anategemea kuingiza gari mpya na lenye thamani kubwa sana ukiachilia mbali Prado analomiliki hivi sasa,Pia msanii huyo ameweka wazi kuwa anamalizia mjengo wake ambao umebakia hatua ndogo sana kukamilika na soon atahamia huko na familia yake kwa sasa msanii huyo ana miliki Toyota prado na Alteza aliyomnunulia mama yake.

Mashabiki wa diamond

Mashabiki wa Diamond Waliofurika kupata show
The super stars tz inapongeza sana Diamond na kumtaka kukaza buti na asife moyo kwani bado anasafari ndefu sana ya muziki wakehivyo asilewe sifa wala asiumizwe na yanayotokea kwani hata fid Q alisema usuperstar mzigo wa mwiba ukiubeba utaumia.


 

1 comment:

  1. ki ukweli kabisa ni kufilisika ki fikra wanalijua hilo wanashindwa kuangalia anajituma kiasi gani kutafuta pesa wabongo noma ndio mana hatuendelei mwacheni mtoto wa watu afanye yake

    ReplyDelete