Sunday, March 10, 2013

WEMA SEPETU APATA AJALI, amgonga mtembea kwa miguu Gari la wema likiondoka maeneo ya ajli hiyo
Wema Sepetu amepata ajali mbaya baada ya gari ambalo alikuwa akiliendesha aina ya Audi Q7 kuacha njia na kugonga gari lingine kisha kumgonga mtembea kwa miguu.
Tukio hilo ambalo lilivuta umati wa watu lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita maeneo ya Makumbusho, jijini Dar ambapo ilidaiwa kuwa Wema alikuwa katika mwendo wa kasi na kushindwa kulimudu gari hilo barabarani.
Ajali hiyo ilisababisha foleni na baadhi ya vijana wanaosadikiwa ni vibaka kuanza kumzingira.
Kwa mujibu wa shuhuda aliyeomba hifadhi ya jina, inawezekana alikuwa na mawazo mengi kichwani kwani licha ya kuwa kwenye mwendo wa kasi, hakukuwa na sababu ya wazi iliyosababisha aache barabara.
Boneti la gari hilo likiwa limeumia baada ya ajali hiyo
“Yaani mi nahisi alikuwa na mawazo mengi au alikuwa ‘amepata’ kidogo,” alisema shuhuda huyo aliyedai aliona mchezo mzima.
Baada ya kugonga, ilidaiwa kuwa mwigizaji huyo alishuka kwenye gari na kutaka kumpiga
vibao mtembea kwa miguu huyo lakini ghafla watu waliingilia kati na kumzuia huku wakimuonya kuwa akithubutu wangemshushia kichapo.
“Huyu dada vipi? Ajali amesababisha yeye halafu anataka kumpiga mtembea kwa miguu, angejaribu tu tungemvua nguo hapahapa,” alisema shuhuda mmoja aliyekataa kuchorwa jina lake gazetini.
Paparazi wetu alipotonywa na kufika eneo la tukio,  alilishuhudia gari la mwigizaji huyo likiwa limebondeka kwa mbele huku akiliendesha kulipeleka katika gereji iliyokuwa karibu na eneo hilo.
Hata hivyo, Wema alipomuona paparazi akiwa na vitendea kazi vyake  akimfuatilia kwenye gereji hiyo, aliondoa gari lake haraka ambapo umati uliokuwa ukifuatilia kwa makini tukio hilo ulimzomea. Haikufahamika alilipeleka wapi.    
credit-globalpublishers

No comments:

Post a Comment