Wednesday, March 27, 2013

WEMA SEPETU AWAPONDA WANAUME WANAO MTUMIA KAMA NGAZI...ASEMA HANA NAFASI HIYO TENA

Wema sepetu akiwa katika ofisi yake
Msanii wa filamu tanzania wema sepetu amesema kuwa sasa amejipanga kuhakikisha kila anachokifanya kinakuwa cha faida kwake kwani ule muda wa mchezo haupo tena kwake.

Akipiga stori na the super stars tz wema amesema kwa kipindi cha nyuma alijikuta akipoteza muda wake mwingi kwa vitu ambavyo havina umuhimu  wala faida katika maisha yake hivyo amejifunza mengi sana na sasa amejipanga kikamilifu kuhakikisha kila anachokigusa kwake ni faida na kwamba hata kubali kupoteza tena muda wake bure.

Moja ya chumba cha ofisi ya wema
Kwasasa wema anamiliki kampuni yake yenye makazi yake mwananyamala koma koma na kwasasa wema anajipanga kwa ajili ya kuanza kuachia filamu zake chini ya kampuni yake hiyo,kampuni ya wema imeshaanza kutowa ajira kwa watu wasiopungua kumi na bado anaendelea kuajiri watu kwa ajili ya kuimarisha kampuni yake

Wema sepetu akiwa na chidy class
Mmoja wa wafanyakazi wa wema chidy classic amesema kwa upande wake anafurahiya kufanya kazici katika kampuni hiyo na kusema wadau wategemee mazuri kutoka katika kampuni hiyo ambayo inaaminika ndio kampuni ya filamu hapa bongo yenye ofisi za kisasa kuliko kampuni nyingine,Kusema kweli wema kajipanga sana kwani kwa sasa ameagiza vifaa vya kisasa vya filamu kuacha hivi unavyoviona nadhani vitaingia katikati ya wikii ijayo vikifika nataka ujue hakuna kampuni itakayoshindana na wema katika vifaa kwa upande wa wawsanii Alisema mmoja wa wafanyakazi katika kampuni hiyo

Chumba kingine cha ofisi ya wema
Wema ameweka wazi maisha yake ya kimapenzi na kusema anaamini mwanaume aliyenaye hivi sasa ni mwanaume mwenye mapenzi ya kweli kwake na wala si mwanaume wa magazeti bila kubainisha au kuweka wazi maana halisi ya neno mwanaume wa magazeti,wema ameonyesha kumsifia mwanaume wake huyo na kusema ni mwanaume muelewa na anaamini kwasasa kapata mtu ndio maana kwasasa katulia na haitaji tena skendo

Sehemu nyingine katika ofisi ya wema katika kampuni hiyo
Msanii huyo aliendelea kuweka wazi mbele ya thesupestarstz kuwa mwanaume wake hataki kabisa habari za kuandikwa katika vyombo vya habari na ndio maana huwa hakuna kashifa kwa kipindi hichi ambacho nipo naye nataka mashabiki wangu wajue kashfa zilizokuwa zikiniandama ni kwasababu sikujijua kama wengi wanataka kunitumia kama ngazi na nilipojua nimejiondoa na ndio maana nikataka niwe na mtu ambaye hana haja na kujulikana na wala haitaji ustaa wangu na mungu amenijalia nimempata alisema wema wakati akipiga stori na the super stars tz.

Huyo ndio wema
Tunampongeza wema kwakujitambua na tunaamini hawezi kurudia makosa na kusema kweli wema kabadilika sana na ni mtu ambaye ukikaa naye unajua ameanza kujipanga zaidi kikazi Hongera tena na tena wema nadhani ndio kitu pekee jamii na wadau wa kazi zako wanataka uwe.

No comments:

Post a Comment