Sunday, April 07, 2013


AIBU:BINTI AVUA NGUO CLUB NA KUTEMBEA UCHI

Hili ni tukio la aina yake lililo tokea usiku wa kuamkia jana katika club maarufu hapa katikati ya jiji ambapo binti mmoja ambae jina lake halikuweza kufahamika mara moja alijikuta akitia aibu katika club hiyo na kusababisha umati wa watu kujaa katika eneo hilo kushuhudia vihoja vilivyo kuwa vinafanywa na binti huyo baada ya kulewa chakali na kuvua nguo kisha kubaki na chupi na kuanza kuwa distabu wateja wengine walio kuwepo mahali hapo wakipata moja baridi moja moto.
Akihojiwa na mwandishi wetu mmiliki wa club hiyo ambae alikataa jina lake lisitajwe alifunguka na kusema "kwa kweli sio utaarabu kabisa kitendo alicho fanya huyu binti hii ni sehemu ya kazi nategemea kazi hii kuji ingizia kipato,sasa mtu anapokuja na kuanza kufanya fujo kwa kweli tunashindwa kumuelewa hata kama umekuja hapa kustarehe kwa pesa zako kumbuka heshima ni kitu cha bure".

Binti huyo aliyefika kwenye club hiyo na jamaa mmoja aliye fahamika kwa jina la jamali alijikuta akiondoka eneo hilo peke yake baada ya jamaa aliyekuja nae kumkimbia baada ya binti huyo kuvua nguo na kuanza kutembea uchi.

No comments:

Post a Comment