Thursday, April 18, 2013

ANGALIA PICHA MBALI MBALI KILE KILICHOJIRI HUKO ZANZIBAR KATIKA MSIBA WA NGULI WA MUZIKI WA TAARABU BI KIDUDE BINT BARAKA

Gari lililokuwa limeubeba mwili wa msanii mkongwe wa muziki wa tarab, marehemu Fatuma Binti Baraka 'Bi. Kidude', likiusafirisha kutoka katika Kijiji cha Kihinani na kuupeleka nyumbani kwake Rahaleo kwa matayarisho ya mazishi yatayofanyika kesho mchana katika Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja. (Picha zote kwa hisani ya Othman Maulid wa ZanZinews)

Ndugu, Jamaa na marafiki, wakiubeba mwili wa marehemu Bi. Kidude wakati ulipowasili nyumbani kwake, Rahaleo kwa ajili ya matayarisho
ya mazishi yatakayofanyika kesho Kijiji cha Kitumba, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.

1 comment: