Monday, April 08, 2013

.AUNT FIFI MTUNZI WA FILAMU YA SENIOR BACHELOR YA JB .... ATOA HUDUMA YA UPONAJI BUREEE!
                                         .Aunt Fifi mwigizaji na mwanamaombi Swahiliwood.

MWIGIZAJI wa filamu Swahiliwood Tumaini Bigirimana ‘Aunt Fifi’ hivi sasa anaombea wagonjwa na wale wenye shida mbalimbali anasema kuwa anasaidia watu kwa njia ya maombi Fifi amesema toka aokoke amekuwa akiwasaidia watu wenye shida, maradhi wanaofika nyumbani kwake au baada ya kuwafuata walipo na ni huduma anayoifurahia.

“Namshukru Mungu kwa huduma ya uponaji nimekuwa nikiwaombea watu mbalimbali ikiwa waliokoka na na hata wale ambao bado hawajaokoka lakini wanampenda Yesu, na Mungu ameonyesha njia kwangu na ni huduma nzuri sana kwangu hata kwa wale wanaokwa jina la Bwana Yesu aliye hai, pia naandika filamu ya wokovu,”anasema Aunt Fifi.
.Aidha msanii huyu mtunzi mahiri wa filamu nchini pamoja na huduma hiyo bado anaendelea na uigizaji na kuandaa filamu na amesema kuwa yeye pamoja kuwa mtu wa Mungu haimzuii kuigiza na kuandika filamu za kidunia kwani ni sehemu ya uhubiri wa neno la Mungu, wakati huo huo msanii Fifi yupo katika mikakati ya kuzindua kitabu chake cha Migogoro ya Ndoa.

Fifi ndio mtunzi wa filamu ya Senior Bachelor aliyoigiza msanii nguli katika tasnia ya filamu Bongo Stephen Jacob ‘JB’ na kujizolea umaarufu na kumpatia tuzo.

No comments:

Post a Comment