Tuesday, April 02, 2013

BAADA YA KUWAPA MAKAVU LIVE CLOUDS FM, LADY JAY DEE KUFUNGUA KITU CHAKE CHA RADIO "KWANZA FM".

Baada ya kutoa makavu live kwa radio ya watu(people's station)/Clouds fm radio kuwa wana upendeleo kwa kupiga nyimbo za watu wao tu na sio za wasanii wa watu wanaopendwa na watu, ikiwemo wimbo wake mpya wa Joto hasira kutokupigwa katika radio hiyo Lady Jay Dee yupo mbioni kufungua kituo chake cha Radio kitakachoitwa KWANZA FM pengine ili kusaidia wanamuziki wengi hasa wachanga ambao ni shida kusikika hewani mara nyingi hata kama nyimbo zao ni nzuri. Lady Jay Dee jana ali-tweet "Kwanza FM coming soon, Yangu mwenyewee". Mwanamuziki huyo anayeheshimika katika nchi za Afrika mashariki na aliyefanikiwa kupitia kazi zake za muziki anaonekana alikuwa anaumizwa na jambo hilo la ubaguzi katika kupita nyimbo za wasanii redioni kwa muda mrefu ila alikuwa anajipanga sawa sawa hivyo kwa sasa yupo tayari kwa vita yeye kama Komandoo Binti Machozi aliandika "Huwezi kuanza mapambano km hujajizatiti, si utapigwa ufe.? Vita ni pale tu unapokuwa tayari. Sikuwa tayari huko nyuma ndio maana sikuongea".

Huyo ndiye Lady Jay Dee a.k.a Komandoo Binti Machozi ambaye kabla ya vita ni lazima ajipange na kujizatiti vizuri kama tweet zake zinavyojieleza

No comments:

Post a Comment