Sunday, April 28, 2013

FATAKI ANASWA LIVE NA MWANAFUNZI GESTI WAKIWA UCHI WA MNYAMA
MfanyabiAshara ‘alwatani’ Bongo, mkazi wa jijini Dar, Allain Tajiri amekumbwa na skendo nzito baada ya kufumaniwa na mwanafunzi wa sekondari wa kidato cha pili mwenye umri wa miaka 16.

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Jumatano ya Aprili 24, mwaka huu katika chumba namba 107 kwenye gesti iitwayo Jamboz iliyopo Kinondoni jijini Dar.

Habari za uhakika zilieleza kuwa tukio hilo lilikuwa ni mtego baada ya walezi wa denti huyo kunasa mawasiliano ya mfanyabiashara huyo akimrubuni binti yao.

Katika mawasiliano hayo, Tajiri alimtaka denti huyo wa sekondari moja iliyopo Kibamba, Dar (jina linahifadhiwa kwa sababu maalum za weledi wa uandishi wa habari), wakutane kwenye gesti hiyo kwa ajili ya kuimomonyoa amri ya sita.

Baada ya walezi hao kuufuma ujumbe kwenye simu ya binti yao, walimuwekea doria bila mwenyewe kujijua na ulipokaribia muda waliokubaliana kukutana gesti, denti huyo aliaga anakwenda ‘tuisheni’.

Huku mwandishi wetu wakiwa ‘stendibai’, kitendo cha binti huyo kuaga muda huo kilianza kuonesha dalili za mtego wa walezi kukaribia kukamilika.

Waandishi wetu ndiyo waliokuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kujibanza wakiwa na picha za wawili hao ambapo walimshuhudia mfanyabiashara huyo akifika kaunta na kuagiza maji makubwa na kuyanywa hadi yakaisha kisha kuelekea kwenye dirisha la mapokezi ya gesti hiyo.
Ilidaiwa kuwa yale maji aliyokunywa chupa nzima alilenga kuwa fiti kwa ajili ya ‘gemu’ na ‘kadenti hako’.


Mmoja wa waandishi wetu naye alijisogeza kwenye dirisha hilo akijifanya kutaka chumba na kumsikia mhudumu akimpa Tajiri chumba namba 107 na kumuonesha kilipo.

Ghafla binti huyo naye alifika mapokezi akiwa na sare za shule ambapo alimkuta paparazi wetu akiendelea kuzuga kwa kutaka kukagua chumba kizuri kabla ya kulipia.

Dakika chache baada ya Tajiri na denti huyo kuingia chumbani, mwanausalama mmoja alitangulia akifuatwa na mwandishi wetu na ndugu wa denti huyo ambapo waliomba kukagua chumba hicho kwa kuwa kulikuwa na binti yao.

Waliporuhusiwa waliingia na kugonga chumba ambapo jamaa huyo alifungua, wote wakakutwa wakiwa watupu huku mfanyabiashara huyo akiwa kwenye harakati za kuvaa ‘kinga’ au ‘dawa ya penzi’ baada ya kumchezea mtoto wa watu.

Tukio hilo lilivuta hisia za jazba kwa umati uliofurika ghafla kwenye eneo hilo huku kila mtu akilaani kitendo cha jamaa huyo kumkatishia denti huyo masomo na kumpeleka gesti kwa ajili ya ngono.

“Fikiria wewe kama mzazi unalipa ada mtoto wako asome halafu mtu mwingine kwa makusudi anamwachisha masomo na kumpeleka gesti wakafanye ngono! Kweli inauma sana, kila mzazi anatokwa na machozi,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo baada ya kuibuka kwa varangati gesti hapo.Kwa upande wake, dada mlezi wa anayemsomesha denti huyo (jina tunalo) alijikuta akimnasa makofi mfanyabishara huyo na kuzua timbwili zito kutokana na kupandwa na hasira ya ajabu.


Katika vuta nikuvute, ghafla jamaa huyo alifanikiwa kuwachoropoka na kuingia mitaani akitimua mbio hivyo kutoa kazi nyingine ya kuanza kumsaka upya ili afikishwe kwenye mkono wa sheria.

No comments:

Post a Comment