Tuesday, April 16, 2013

HII NDO MOVIE MPYA KUTOKA KENYA INAYOGHARIMU KARIBU MILLION MIA 600 ZA KITANZANIA NA KUSITISHA BAJETI NCHINI KENYA.Filamu mpya ya Jack Zollo - My Life in Crime, kutoka huko nchini Kenya, imepangwa kuanza kufanyika mwezi wa 9, na kitu kikubwa kinachowapa watu wengi msukumo, ni bajeti yake ya shilingi milioni 35 za Kenya ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 600 za Kitanzania kuitengeneza.

Filamu hii itabeba nyota kama vile Melvin Alusa Ainea Ojiambo, Lenana Kariba, Jeff Koinange na pia star wa filamu wa Naijeria Jim Iyke atapewa mashavu ndani yake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo, Filamu hii itafanyika kwa sehemu huko Mombasa na pia Nairobi ambapo katika sehemu ya maandalizi pia, Jim Iyke anatarajiwa kutua mwezi mmoja kabla ya shughuli nzima kuanza ili kuanza kujiweka sawa na mazingira.

No comments:

Post a Comment