Monday, April 08, 2013

IRON LADY WA UINGEREZA AFARIKI DUNIAAliyekuwa waziri mkuu wa zamani wa Britain,Margaret Thatcher "Iron Lady" amefariki dunia leo asubuhi.Mama huyo ambaye amefariki dunia leo asubuhi,amefariki akiwa na umri wa miaka 87.

Kwa huzuni kubwa Carol Thatcher na Mark ambao ni watoto wa marehemu wa aliyekuwa waziri mkuu wa Britain wa karne 20,walitangaza kuwa mama yao aliaga dunia kutokana na stroke leo asubuhi na kuongeza kuwa taarifa zaidi itatolewa hapo baadae

Taarifa ambazo zilipatikana kutoka kwa mwanae wa kike, zilisema kuwa mama huyo alikuwa akisumbuliwa mara kwa mara na matatizo madogo madogo ya stroke na mwaka 2012 alifanyiwa operesheni ya kibofu kilichodaiwa kuwa kilikuwa kinaongezeka.

Katika uhai wake na mambo ya siasa, Margaret alikuwa akijulikana kama Iron lady na aliiongoza Great Britain kuanzia mwaka 1979 mpaka mwaka 1990 kitu amabcho kinasemekana kwamba ndie waziri mkuu aliyeongoza great Britain kwa muda mrefu zaidi mpaka sasa kushinda mawaziri wengine wakuu wote waliopita.

May God rests his soul in eternal peace

No comments:

Post a Comment