Tuesday, April 30, 2013

JB AWEKA WAZI MKOA ATAKAOGOMBEA UBUNGE 2015
 
 HATIMAYE nguli wa sanaa za maigizo Bongo, Jacob Stephen Mbura ‘JB’ amelianika jimbo atakalogombea ubunge mwaka 2015.
JB aliyaongea hayo mwanzoni mwa wiki hii, jijini Dar es Salaam ambapo
alisema macho yake yote yapo Mkoa wa Dar es Salaam ambao una majimbo nane. 

JB: Niliposema natangaza kugombea ubunge mwaka 2015 wengi waliamini ni maneno tu, lakini nia yangu ni sahihi. Nitagombea na leo nasema jimbo langu lipo Mkoa wa Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa, jimbo atakalogombea litaendelea kubaki kuwa siri ya moyo wake na meneja wake wa kampeni ambaye hakupenda kumtaja jina.
Majimbo yanaounda mkoa wa Dar es Salaam katika uwakilishi bungeni ni Ukonga, Ilala, Kinondoni, Segerea, Kawe, Kigamboni, Ubungo na Temeke.

Kiukweli umefika wakati sasa wakurudisha fadila kwa mashabiki wangu nahitaji kuwatumikia  kwani na amini nikifanya hivyo hata kwa mungu nitapata baraka alisema msanii huyo mwenye mashabiki wengi sana 
Jb aliendelea kuieleza thesupestarstz kuwa kugombea kwake ubunge kunaenda sambamba na hali halisi anayoiona kwa wananch watanzania na kuongeza kuwa sasa tunatakiwa kuwa na hofu ya mungu kwa wananch wetu wanaotuchagua kwa kura nyingi wakiamini wamepata mkombozi matokeo yake wewe unawageuka ki ukweli inauma sana.

Thesuperstarstz imeongea na baadh ya wasanii wenzake kutaka kujua wanalichukuliaje swala hilo ambapo wengi wameonyesha kumkubali jb na kusema kama atafanikiwa kuwa mbunge basi utakuwa ni wakati mzuri sasa kwa wasanii kupata mkombozi 

No comments:

Post a Comment