Monday, April 08, 2013

JINI KABULA: "JACK CHUZ NI MALAYA NA ALINIIBIA MPENZI WANGU.....NAWASHANGAA WANAOSEMA KUWA HUWA NAMTONGEZEA WANAUME"

 


MWIGIZAJI aliyeng’ara kupitia Tamthilia ya Jumba la Dhahabu, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, ameirarua ndoa ya mwigizaji mwenzake, Jacqueline Pentzel ‘Jack Chuz’ baada kuambiwa amehusika kuiunganisha ndoa hiyo.

Jini Kabula alifikia hatua ya kufunguka hayo hivi karibuni baada ya Jack Chuz kufunga ndoa na Gadna Dibibi kisha kushushiwa lawama na mwanamke ambaye alizaa na mwanaume huyo wa Jack.

 Chanzo kilichoomba hifadhi ya jina kilidai kuwa baada ya Jack Cho umesababisha Gadna kumuacha mwanamke aliyezaa naye na kumuoa Jack.

 “Jini Kabula amechukizwa sana na maneno hayo kwani hata yeye hakumkuwadia Jack, hasira zilipompata ndipo alipotoa siri ambayo hajawahi kuitoa kwamba hata yeye aliwahi kuporwa mume na Jack,” kilisema chanzo hicho.

Akionesha hisia zake kuhusiana na tuhuma hizo za ukuwadi, Jini Kabula alisema hataki kulaumiwa kwani hana tabia za aina hiyo.

Nachukizwa sana na watu wanaosema nimemshawishi Jack kuolewa wakati nina maisha yangu na yeye ana maisha yake, ana uamuzi wake kwenye maisha yake, naomba kuwa mimi si mzazi wa Jack wanikome.Mimi siyo kuwadi na wakae wakijua yule ni Jack na mimi ni Miriam, hivyo ni vitu viwili tofauti. Maisha yake hayanihusu na huyo demu aliyezaa na Gadna anashangaa nini Jack kuolewa na mzazi mwenzie wakati mimi sishangai kwa kuwa Jack aliwahi kunipindua kwa baba mtoto wangu Chuz,” alisema.

No comments:

Post a Comment