Sunday, April 21, 2013

JUMA NATURE ATIMULIWA EATV BAADA YA KUINGIA AKIWA AMEVAA KANDAMBILI.....

Msanii mkongwe na maarufu nchini, Juma Kassin Kiroboto, aka Nature, ameonyesha kukerwa na kitendo  cha  kutimuliwa  jana usiku katika kipindi cha burudani cha televishen inayotizamwa africa ya mashariki alipokuwa akifanya nao interview. 

Nature alionekana akiwa amevaa kawosh na ndala na mara baada ya mahojiano mafupi ya mwanzo  mtangazaji alisema watarejea baada ya mapumziko mafupi  na ndipo Nature hakuonekana tena.
  Kilichotokea kwa mujibu wa Nature mwenyewe, ni wakati wa mapumziko hayo, mtangazaji wa kipindi hicho alimfuata na kumuambia kuwa hataendelea na interview tena kwasababu ya mavazi aliyokuwa kavaa ambayo ni ndala na kawosh. kuonyesha kukerwa kwake na ishu hiyo Nature aliamua kuandika yafuatayo  kupitia ukurasa wake wa facebook....

"hivi kwa mfano angekuwepo mzungu pale na kavaa ndala wangesitisha mahojiano na kuvaa kaoshi ni tatizo....

kunywa nimekunywa bt kuna baya nimeliongea na hivi  kweli we  kama muandishi wa habari unaruhusiwa kuvaa vile kisheria kama yule mtangazaji nimeboreka kinoma na ikiwezekana nasitisha kuanzia ssa kupeleka ngoma zangu pale siitaji interview
alisema juma kwa hasira

12 comments:

 1. Hiyo noma juu Nature yupo juu tu sana

  ReplyDelete
 2. Hiyoo mibangiiiiii

  ReplyDelete
 3. Bro ulibugi japo raia wanakuelewa..

  ReplyDelete
 4. Nilazima ujue wewe ni role modal au mfano kwa jamii, kuanzia uvaaji nguo ,kuongea na matendo. Wasanii wengi halijui hilo. Walichofanya nawaunga mkono

  ReplyDelete
 5. Kwani mpaka wanakufanyia enterview hadi wanafikia mapumziko walikuwa hawakakuona?

  ReplyDelete
 6. yeap safi sana yu a legendary bana wasikuzingue....kuwa proud na style za home ei wanakufukuza huo no ulimbukeni....

  ReplyDelete
 7. Never mind wapumbavu hao; ilo li mtangazaji ni li nani; mijitu mingine jaman?? Angrrrr!

  ReplyDelete
 8. Hee naona mwanzo hakukuona, labda mtangazaji alivaa miwani ya mbao!! kuivua tuu Oooh!! kiroboto katupia kawoshi na kandambili pale kati!!

  ReplyDelete
 9. wale wote wanao mshauri ni wajinga kama kavaa ovyo asemwe when atachange ndo mana hapati show hata hapo Nairobi kisa kuwa rough acheni upuuzi kama kafanya ovyo asisemwe kisa nature MSONYO. Na kukataliwa kuendelea na interview ni kumsaidia mana kipindi kinaangaliwa na wengi angeendelea kuhojiwa angeshusha hadhi ya TV na yake kwa siku moja wkt mtu kajenga jina la station yake kwa miaka.
  its time to change mbona wanamuziki wa nje wanavuta mibangi na wanavaa fresh

  ReplyDelete
 10. SAFI SANA EATV KWANI JUMA NATURE HAJITAMBUI...
  ASILI YAKE NI MCHAFU HIVYO UCHAFU WAKE HUKO HUKO SIO KWENYE TV....
  EATV JINA KUBWA, WASANII KAMA KINA JUMA JIEPUSHENI NAO.....

  ReplyDelete
 11. SAFI SANA EATV KWANI JUMA NATURE HAJITAMBUI...
  ASILI YAKE NI MCHAFU HIVYO UCHAFU WAKE HUKO HUKO SIO KWENYE TV....
  EATV JINA KUBWA, WASANII KAMA KINA JUMA JIEPUSHENI NAO.....

  ReplyDelete
 12. hv mbona wazung huwa wanavaa ndala n kuingia sehem yoyote?y us muachen bhana ameamua ilimrad havunji sharia za nchi n sawa afanye anavyotaka bas waweke sharia ukiwa na interview uvae nguo fulan

  ReplyDelete