Tuesday, April 09, 2013

DIAMOND KIGEUGEU! AGEUKA KAULI YAKE MWENYEWE ALIYOSEMA WASANII WA TZ WANAFAIDIKA NA KAZI ZAO. Hivi karibuni mwanamuziki Diamond akiwa huko Kigoma kwenye ikulu ndogo aliulizwa kama wasanii wa Tanzania wanafaidika na kazi zao au lah? na mwanamuzikii huku wakisema Diamond hana upeo amezuzuka na show za kulipwa million 10 wakati angekuwa bilionea kama wanamuziki wenzake kutoka Nigeria au nchi nyingine za kiafrika walio matajiri kama serikali ya Tanzania ingethamini kazi za wasanii kwa vitendo na siyo maneno matupu.

Pia kampuni moja hivi karibuni ilisema kuwa Diamond ndiye mwanamuziki anayeongoza kwa kuuza ringtone na msemaji huyo kusema kama angekuwa Diamond angetengeneza pesa nyingi sana kuliko sasa sababu muziki wake unauzika. Lakini mwanamuziki huyo amegeuka kauli yake ya awali kuwa wasanii wanafaidika na kazi zao na sasa ameigeuzia kibao serikali hiyohiyo aliyoiambia wanamuziki wanafaidika na kazi zao kuonyesha kuwa mwanzoni hakuwa amejipanga au aliogopa kusema ukweli mbele za waheshimiwa.

chanzo swahiliworldplanet

No comments:

Post a Comment