Tuesday, April 09, 2013

KAULI YA RAISI WA KWANZA WA ZNZ ABED KARUME YAANZA KUFANYA KAZI..HII NI BAADA YA BAHARI KUTAFUNA KISIWA CHA ZANZIBAR KWA KASI.

 
KUNA kila dalili kuwa maono ya muasisi wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Abeid Amaan Karume, kuwa iko siku kisiwa hicho kitajaa na kulazimika kupata ardhi Tanzania Bara, kuanza kutimia. Maono hayo yametajwa kuwa miongoni mwa sababu za Karume na Baba wa Taifa, Julius Nyerere, kuunganisha nchi hizi mbili katika Muungano wa kihistoria uliodumu miaka 49 sasa, mbali na sababu ya udugu kati ya watu wa Bara na Visiwani hata kabla ya uhuru

Gazeti hili lilipata kumnukuu mmoja wa mawaziri waliokuwapo wakati Muungano unaasisiwa, Hassan Nasoro Moyo, kwamba Mzee Karume aliwaambia Zanzibar ni kisiwa kidogo na kinaliwa na bahari na Tanzania Bara ni nchi kubwa, hivyo baada ya Muungano, Wazanzibari watapata fursa ya kupata ardhi na kuishi Bara.
Maono hayo ya waasisi wa Muungano wa 1964, yameanza kudhihirishwa na Ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, na taarifa za Serikali kuhusu upatikanaji wa maji na kupotea kwa visiwa vidogo.

Ripoti hiyo kuhusu idadi ya watu iliyotolewa wiki iliyopita, inabainisha kuwa Zanzibar imejaa na sasa wastani wa wananchi wake kwa eneo, umezidi wastani wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment