Tuesday, April 09, 2013
MA  STAR WAGOMBEA NGUO ZA BONGE LA BWANA ZA JB.JACK WOLPER AWA WA KWANZA


              Mdau wa Filamu Gertude akiwa na fulana ya JB Bonge la Bwana.

BONGE la Bwana ndio jina linalovuma kwa msanii wa filamu Bongo Jacob Stephen ‘JB’ kwa sasa Jb ameingia rasmi katika ujasiriamali baada kuzindua mavazi yake ya JB Wear na kuwauzia wapenzi wa filamu wanaopenda kumuunga mkono katika harakati zake za filamu Bongo, JB anasema kuwa naye anaungana na wasanii wakubwa Duniani ambao pamoja na kazi za Sanaa pia umiliki biashara nyingine.

.
                                 JB nyota wa filamu Swahiliwood

JB anakuwa msanii wa kwanza wa filamu kuuza nguo zenye alama yake baada kuona wasanii wa kizazi kipya Bongo fleva wakiwa na nguo zao kama vile AY na Gangwe Mob waliwahi kufanya hivyo, JB anatamba na filamu kali kama Senior Bachelor, Nakwenda kwa Mwanangu, Regina na filamu nyinginezo zilimpa uigizaji bora katika  filamu.

   


Jack Wolper, Marco Kilo, Getrude, TC waking'aa kwa kupiga JB Wear.


“Nafahamu kuwa kwa sasa jina langu katika sanaa limekuwa zaidi na ninahitaji kuwa na lebo yangu kwa ajili ya watu wangu ambao kila siku wananunua kazi zangu baada ya kupokea maoni nimeamua kutangaza mavazi yangu JB Wear na JB Bonge la Bwana tayari T-Shirt na Top zimeingia na zinapatikana katika ma duka mbalimbali,”anasema JB.
 .
            Jack Wolper, Marco Kilo, Getrude, waking'aa kwa kupiga JB Wear.


T-shirt hizo kwa sasa zinagombewa na nyota wa filamu kibao kulingana na ubora wake zilivyotengenezwa na kuvutia mbunifu wa kazi hiyo ameonekana kuwa makini katika ubunifu wake, kwa wale ambao hawawezi kufika katika maduka zinakopatikana JB Wear wanaweza kuwasiliana na wauzaji kwa namba .0713 37 21 94….0766 50 45 60 na utapata mzigo ulipo USIKOSE BONGE LA BWANA.

No comments:

Post a Comment