Friday, April 05, 2013

MFANYABIASHARA ALIYEUAWA CHINA NA MAITI YAKE KUKAA MONCHWARI MWAKA MZIMA AZIKWA JIJINI MWANZA...!!


MFANYABIASHARA, Mkumbukwa John Shayo (37) (pichani) aliyefariki katika kifo chenye utata nchini China amezikwa Jumatano iliyopita na kulifanya Jiji la Mwanza kutawaliwa na majonzi.
Umati wa watu ulihudhuria mazishi hayo nyumbani kwa bibi wa marehemu, Mabatini kisha kuelekea katika Makaburi ya Buzuruga, Nyakato na kila mtu alionekana kujawa na huzuni.
Hata hivyo, mazishi hayo yaliathiriwa kidogo na mvua iliyofanya baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki washindwe kuuaga mwili wa marehemu.
Mkumbukwa alifariki China na maiti yake kuhifadhiwa hospitali kwa takriban mwaka mzima na serikali ya nchi hiyo huku mkewe, Neema Majukano pamoja na rafiki wa marehemu aitwaye Haji Msongore wakilaumiwa kwa kushindwa kutoa taarifa mapema juu ya kifo hicho.
Aidha, utata umegubika kifo cha Mkumbukwa kufuatia rafiki huyo wa marehemu ambaye mara ya mwisho walikwenda wote nchini China na kwasasa  anadaiwa ndiye aliyemuoa mke wa marehemu, Neema.huku maiti ya marehemu mkumbukwa ikisota kwenye friji kwa mwaka mzima sasa

No comments:

Post a Comment