Monday, April 15, 2013

MIMI SIKUMBAKA SHILOLE BALI ALINIPA PENZI LAKE KWA HIARI"...MAKALA


MZAZI mwenziye na staa wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Makala Elias amembomoa staa huyo na kumwambia aache kuungopea umma kuwa alibakwa wakati waliishi naye kinyumba. 

Akiongea na mwandishi wetu, Makala aliweka wazi kuwa anasikitika anapomsikia Shilole akisema kwamba alipata ujauzito baada ya kubakwa wakati walioana na kuachana miaka ya nyuma kabla staa huyo hajawa maarufu.

“Namsihi Shilole aache kusambaza taarifa kwenye vyombo vya habari na kuwafanya Watanzania wamuone mtoto aliyenaye alimpata kwa njia ya kubakwa wakati alikuwa ameolewa na mimi,’’ alisema Makala ambapo Shilole alikataa kuzungumzia juu ya ishu hiyo akidai ameshazungumza mara nyingi.

No comments:

Post a Comment