Monday, April 15, 2013

MWANAUME MMOJA ANUSURIKA KUPOTEZA MAISHA BAADA YA KUFANYA MAPENZI NA MWANAMKE MMOJA BILA YA KUMLIPA PESA YAKE STORY KAMILI HAPA.


Tukio hilo lililokusanya umati lilijiri maeneo ya Mwenge jijini Dar mishale ya saa 10 usiku ambapo mwanaume mmoja  mkazi wa Tegeta, alikiri kupokea kipigo almanusra apoteze uhai kutoka kwa mwanamke huyo aliyetambuliwa kwa jina Neema Samson, mkazi wa Buguruni.

Habari za uhakika ni kwamba Neema alidai kuwa mwanaume huyo ambaye ni mume wa mtu ana tabia ya kumtafuta yeye kwa ajili ya huduma ya mapenzi lakini akishakidhi matakwa yake huwa hataki kutoa fedha kama wanavyokubaliana.
“Namjua ni mume wa mtu, ni kweli nimefanya naye mapenzi na kama hamuamini niwaoneshe (huku akipandisha nguo na kubaki mtupu), nataka buku kumi na tano yangu la sivyo namtoa roho,” alisikika Neema akifoka kwa hasira.
Wakiwa eneo la tukio, mjumbe wa nyumba kumi alifika na kuwashuhudia wakigaragazana mchangani ambapo Joseph alidai kuwa Neema alimwibia simu yake aina ya Nokia.

Kwa upande wake, mjumbe wa nyumba kumi alijitahidi kwa uwezo wake wote kuwaamua lakini ilishindikana kwani Neema aliendelea kumkwida Joseph akidai ujira wake kwani tayari simu aliyokuwa ameisunda kwenye nyeti, alikuwa ameshanyang’anywa na wasamaria wema.

Wawili hao waliendelea kuvutana hadi wasamaria wema waliposhirikiana kuwabeba kisha kuwapakiza kwenye Bajaj na kuwapeleleka kituo cha polisi....
No comments:

Post a Comment