Monday, April 01, 2013

NATURE ADHIHIRISHA KUWA YEYE NDIYE MFALME WA TEMEKE AWAFUNIKA VIBAYA TEMBA,CHEGE NA KUNDI LAO

Sir Kassim Juma Nature, kinara wa kundi la TMK Wanaume Halisi akiwanyooshea Mike mashabiki wake usiku wa kuamkia leo katika mchuano wa NANI MFALME ambapo mashabiki walimkubali kuwa Mfalme wao dhidi ya mahasimu wao, TMK Wanaume Family.
Hivi ndivyo ilivyokuwa kwa mashabiki wa TMK Halisi, wakati wote vidole juu...TATU BILA, hata walipopagawishwa na nyimbo kali za TMK Family.
Mhe. Temba akicheza na mashabiki katika mpambano huo wa kukata na shoka
JB wa TMK Halisi akicheza na mashabiki wake pia
Sir Nature (kulia) na Doro..kazini
Mhe. Temba na Chege,,,kazini
..Inspector Haroun akiwa jukwaani akiwakilisha Gangwe Mob kivyake
..Inspector anapoamua kuvua viatu na kupiga shoo peku...
..Chezea Dar Live wewe!
Malkia wa Mipasho, Khadija Kopa akionesha manjonjo yake mbele ya mpiga gitaa wake!
...dogo Lila kutoka kundi la Nature, akiwa ni member mpya wa kundi, akichana mistari vibaya mno....
...dogo Aslay wa TMK Family akiwaimbisha mashabiki
...Profesa jay nae alikuwepo kuwakilisha vilivyo game ya Hip Hop
DJ Jd alikuwepo kwenye mashine kucheza nyimbo za Prof jay na pia kuwaonesha Ma DJ chipukizi jinsi ngoma inavyochezwa!
........shooo wa Wanaume Family ikipamba moto
DJ JD alikuwa kama jaji pia, hapa akimtangaza Nature ndiye Mfalame kama mashabiki walivyoitikia.
...Nature akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mfalme.
PICHA: Richard Bukos na Issa Mnally - GPL

No comments:

Post a Comment