Monday, April 08, 2013

NGUO ZA JB BONGE LA BWANA ZA KIMBIZA SOKONI..MWENYEWE AWASHUKURU MASHABIKI WAKE KWA JINSI WANAVYONUNUA NGUO ZAKE KWA WINGI

Msanii mahiri nchini tanzania jacob stephan amabye amejizolea umaarufu mkubwa sana kutokana na umahiri wake wa kuigiza sehemu tofauti na kuvaa uhusika kulingana na eneo alilopangiwa kuigiza  amezungumza na thesuperstarstz muda mfupi na kuelezea kiundani biashara yake ya mavazi ambayo ameibuni hivi karibuni akiwa na meneja wake.

Akipiga story na thesuperstarstz mapema hii leo jb alisema anamsukuru mungu sana kwani biashara inaenda vizuri na mzigo wa kwanza uliisha hivyo kumlazimu meneja wake kuongeza mzigo mpya wenye ubora wa hali ya juu 
.Msanii huyo ambaye anasema hufarahi zaidi kama utamuita bonge la bwana amesema ametengeza tshart na top zenye ubora mkuba na hivi karibuni utaingia mzigo wa jeans mashati boxer saa mikanda na ma henbage vyote vikiwa na nembo za jb bonge la bwana,jb ameendelea kuieleza thesuperstarstz kuwa chini ya meneja wake ambaye ni marco kilo wamejipanga kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa na mashabiki hawakosi kuwa na jb popote pale.


Akiongea na thesuperstarstz meneja wa msanii huyo Marco Kilo amesema nembo ya msanii huyo mkubwa katika tasnia ya filamu ni yenye ubora wa hali ya juu na wameamua kutoa hiyo kwaajili ya wapenzi wa filamu ambao wanamhusudu sana JB ikiwa kama ni sehemu ya zawadi yao kwa wapenzi wa filamu na wadau wa filamu Bongo
 JB ni kipenzi cha watu, kuna wakati ambao wengi upenda kupiga naye picha wakionyesha mapenzi na msanii wao, kama uongozi tumepokea maoni mengi wakitaka JB aweze kutoa mavazi kwa ajili ya kuitangaza nembo yake ya JB Bonge la Bwana nasi kwa kuheshimu hilo tumefanya hivyo,”anasema Killo.


 

.
Patrick Nyembera - Presenter wa EATV 
 Kwa upande wa mdau mkubwa wa jb Patrick Nyembera - Presenter wa EATV Ameongea na blog hii na kusema kuwa kwa upande wake anamkubali sana jb na ndio maana huwa hakosi kuangali movie zake na amefurahi sana kwakutowa hizo tshart kwani anaamini wadau wengi watazinunua ili kumsapot msanii huyo ambaye ni kipenzi cha wadau na mashabiki wa filamu zetu ndani na nnje ya nchi

 JB Amesema kuwa kwasasa nguo hizo zinapatikana katika maduka ya hapa dar eas salam na baadhi ya mikowa huku lengo likiwa nikusambaa tanzania nzima na kuvuka mipaka katika nchi zote ambazo filamu zetu zimefanya vizuri,kwa upande wa meneja alisisitiza kununua nguo hizo ili kumuunga mkono jb kama mnavyomuunga katika filamu zake alisema kilo. huku akisisitiza pia  Wapenzi wa filamu wataweza kujipatia tishirt, Top na vitu vingine katika maduka mbalimbali ikiwa na alama ya JB bonge la bwana ikiwa katika ubora wa kipekee, tumuunge mkono msanii wetu katika kujiimarisha na kuongeza kipato.

Mwisho jb aliwashukuru wadau wote ambao wamemuunga mkono kwa haraka sana na kununua nguo kwa wingi huku akizidi kuwaomba wasichoke wazidi kumuunga mkono katika nguo na filamu zake huku akisisitiza kuwa anawapenda mashabiki zake kama wanavyompenda na kamwe hatawaangusha hata siku moja kwani bila mashabiki hakuna jb wala jb bonge la bwana

No comments:

Post a Comment