Tuesday, April 09, 2013

"NIMEAMUA KUMSAMEHE LULU MICHAEL....YALIYOTOKEA NAMWACHIA MUNGU"...MAMA KANUMBA

Lulu na Mama wa Marehemu Kanumba

Mama wa marehemu Kanumba Flora Mtegoa amesema amemsamehe msanii Elizabeth Michael 'Lulu' kutoka moyoni .Ingawa bado kesi iko mahakamani, kwa upande wake yeye hana tatizo naye na yaliyotokea anamuachia mungu

Akizungumza katika makaburi ya Kinondoni mara baada ya kumuombea marehemu na kuweka mashada ya maua alisema kuwa yeye ni mkristo safi hivyo hawezi kuendelea kukaa na kinyongo ingawa kila anapomuona msanii huyo humkumbuka mwanaye

Alisema kuwa Kanumba alikuwa zaidi ya mtoto kwake, mume, rafiki, kaka alimfanya kuwa mtu wa karibu sana kwake na alimfanya kuwa karibu kwake na kumzoea kwa kila kitu hali ambayo imemfanya kuwa mpweke mpaka leo

No comments:

Post a Comment