Thursday, April 18, 2013

PONGEZI: H. BABA AINGIZA SOKONI PIPI ZENYE JINA LAKE


H. Baba akionesha pipi zake.

Katika kuonesha kwamba bado ana kiu ya kuona sanaa yake inapanuka  na kuvuma mbali huku akiboresha maisha yake, kukuza kipato na kuongeza ufanisi , msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini H. Baba ameamua kujikita katika biashara kwa style ya kipekee  kwa kuingiza sokoni bidhaa aina ya pipi zenye jina, picha na chata zake, pipi zinazojulikana kwa jina la "H. BABA & FLORA MAPENZI KWA WATOTO". Pipi hizo zilizopambwa kwa picha ya H. Baba katika karatasi ya kuishika pipi, zikipambwa na mfuko wa nylon wenye uzito wa gram 250 uliona picha ya mwanamuziki H. Baba na mwigizaji wa Bongo movie Flora Mvungi  na  zinazo tengenezwa na kampuni ya TANFRIK LIMITED ya Nairobi nchini Kenya, tayari zimeanza kuuzwa kwenye baadhi ya maduka na vibanda mbalimbali vya biashara kanda ya ziwa.
Muonekano wa mbele.
Muonekano wa nyuma.

No comments:

Post a Comment