Wednesday, April 10, 2013

PRINCE RICHARD STAR WA MOVIE NA ALIYEKUA MENEJA WA KANUMBA, ASEMA WASANII WATANZANIA WANAOGAPA KUVUKA MIPAKA KISA KINGEREZA AMBACHO SIO SABABU YA KUWAZUIYA                                   Prince Richard meneja wa marehemu Kanumba.

MTAYARISHAJI na meneja wa wasanii wa filamu kwa Tanzania Nigeria Ghana nchi nyinginezo kama Marekani Prince Richard Nwaobi amewataka wasanii wa filamu Bongo kufuta fikra kuwa kutojua kwao lugha ya Kiingereza ni tatizo linalowafanya washindwe kuwa wasanii wa kimataifa bali watumie Kiswahili kama Lugha kufika anga za kimataifa.

                                 Prince Richard akiwa na Seth Bosco mdogo wa Marehemu Kanumba.

Prince Richard ambaye pia alikuwa ndiyo meneja wa marehemu Kanumba yupo nchini kwa ajili ya kuazimisha kumbukumbu ya nyota wa filamu Swahiliwood Steven Kanumba, akiongea na FC katika mahojiano alidai kuwa mara nyingi amekuwa akiwasili Tanzania kwa lengo la kuwaunganisha wasanii wa Tanzania na nchini nyingine ikiwa ni pamoja na kuingia Hollywood.

Lakini bado hajapata mwitikio kama aliokuwa nao marehemu Kanumba kwani marehemu alikuwa ni nia dhabiti kuinyanyua tasnia ya filamu Swahiliwood alikuwa mpiganaji amabye alipopata fursa hakuwa nyuma katika kupigania tasnia ya filamu Bongo ikuwe na kwenda mbali zaidi nje ya mipaka ya Tanzania.

“Wasanii wa Tanzania wameshindwa kufuata nyayo za marehemu Kanumba kwa sababu ya hofu yao ya kutojua Kiingereza lakini bado wanashidwa kujua kuna wasanii maarufu wengi ulimwenguni hawajui Kiingereza mfano mzuri Bruce Lee ni mtu maarufu kuliko hata Jet Lii ambaye anajua kiingereza na anacheza kama Bruce, mifano mingi kuna filamu kama Slumdog Millionaire ilichezwa na kijana asijua lugha hiyo,”anasema Prince Richard.
.
                                            Prince akipiga story na FC Kimara Temboni.

Pia mtaalamu huyo wa masuala ya filamu alizidi kusisitiza kuwa wasanii wanahitaji kuwa na utawala unaojua wajibu wake katika kuwasimamia wasanii na kuwatangaza pia, nazidi kusema kuwa mataifa kama India yamefanikiwa sana katika tasnia ya filamu kwa kutumia lugha zao, ni fursa kwa wasanii wa filamu kutumia lugha yao ya Kiswahili kutangaza Taanzania.

Prince Richard katika msafara wake ameongozana na wasanii wa filamu kutoka nchini Ghana Nana ambaye ni Komediani, na Amma msanii nayr pia ambao wote kwa pamoja wamegushwa na kuondokewa kipenzi Kanumba marehemu alifariki tarehe 7. Aprili. 2012 kwa kuaguka akiwa na msanii ambaye pia alikuwa naye jirani Lulu

No comments:

Post a Comment