Thursday, April 18, 2013

TAARIFA ZA MWISHO KUZIPATA KUHUSU MSIBA WA BIBI KIDUDE ZNZ

ZNZ 
Mtangazaji Sakina wa Clouds TV ameongea na millardayo.com akiwa Zanzibar sasa hivi Msibani kwa Msanii wa siku nyingi Bibi Kidude na hapa namkariri akisema “Anatarajiwa kuzikwa kesho April 18 2013 Zanzibar saa saba mchana pembeni ya kaburi la Baba yake , japo kuna habari za chini ambazo bado hazijathibitishwa kwamba kuna uwezekano akaagwa kwanza kwenye Uwanja wa Karume alafu azikwe saa kumi jioni”
“Bibi Kidude hakuwahi kupata mtoto lakini nimekutana na kijana mmoja aitwae Baraka ambae kwa sasa umri umekwenda kidogo, anatambulika kama ndio mwanae Bi Kidude kwa sababu alimlea toka akiwa na miezi mitatu, japo maziwa yalikua hayatoki, imefahamika aliwahi kumnyonyesha ziwa lake” – Sakina
Kwa kumalizia, Sakina anasema “Baraka akiwa na umri wa miaka 13 ndio aligundua kwamba Bibi Kidude ni shangazi yake, baba Baraka alimpa Bi Kidude Baraka baada ya kuona hakuwa amepata mtoto, hapa kwenye msiba watu ni wengi sana na inakua ngumu kwa mgeni kujua ni nyumba ipi yenye msiba  

Unaweza kumsikiliza Sakina Mwenyewe akiongea hapo chini, pia millardayo.com itaendelea kukupa habari wakati wowote zinapopatikana, cha kufanya ni kujiweka karibu kupitia facebook.com/millardayo twitter.com/millardayo na instagram.com/millardayo

No comments:

Post a Comment