Wednesday, April 03, 2013
 IRENE UWOYA NA NDIKU WAONYESHA MAHABA UKUMBINI WAKANUSHA KUACHANA WASEMA WAO NI MKE NA MUME  

Msanii wa filamu nchini tanzani na ambaye ni mama wa mtoto mmoja irene uwoya hivi majuzi aliwaziba watu midomo kwa kile kinachonekana kama hana matatizo na ndowa yake kama wengi wanavyotafssiri.

Mwishoni mwa wiki the superstarstz ilishuhudia irene na mumewe ndikumana anayesakata kabumbu nchini rwanda kukumbatiana na kubusiana mbele ya umati mkubwa huku wakionyesha kila dalili za kuwa wamekumbukana sana.

Tukio hilo lilijiri wakati vijana wawili wa bongo movie kupa na jimy mafufu  walipoamua kuowana na wapenzi wao siku moja,walikwa wakiwa ukumbini hapo ndipo uwoya aliposimama na kumkumbatia kisawa

umewe huyo na kuganda kwa dakika kadhaa kifuani kisha yakaanza mabusu mototo wawili hao walionekana kumisiana licha ya maneno yaliyozagaa mtaani kuwa wawili hao wameachana.

The supestars tz ilishindwa kukaa kimya iliamua kumfuata uwoya na kuzungumza naye kuhusu yalionekana pale ukumbini na nini hatima yao Unajua mimi siwezi kuwazuiya watu wasiseme ila mimi najua kuwa mimi na mume wangu tupo pamoja na wala hatujaachana ila kama unavyojua mimi au yeye ni wanadamu kutofautiana lazima japo si pakufikia kuachana ila watu wanapoona vile haswa marafiki zangu wanafki wanazisambaza habari kwa upana kana kwamba ni vita alisema uwoya

Kwa sasa uwoya ameonyesha ukaribu zaidi na mumewe huyo kwani the super stars tz ilimshuhudi uwoya kule rwanda akiwa na mumewe huyo kila mara na kuondowa zile fikra za watu kuwa akifika rwanda wanyarwanda watampiga kwakumuumiza kaka yao badala yake redio,magazeti na tv zote zilitangaza mke wa ndikumna anakuja rwanda huku kila mtu akimsubiri kwa hamu.

Baada ya kupata maelezo ya uwoya the super stars tz iliongea na ndikumana na kutaka kujua msimamo wake kwa mkewe huyo ambapo alisema kwake ni kama hadithi au kusoma riwaya kwani anachojua yeye uwoya bado ni mkewe na wanamlea mtoto wao.muandishi wetu alimkumbusha matukio ya nyuma na kumuuliza kama yalikuwa ya uwongo au yalikuwa ya kuzusha alisema mengi ni ya uwongo tena sana

the super stars tz inawatakia ushindi mkubwa katika vita hii ya maneno na nina imani watashinda tu kwa kuwa alichokiunganisha mungu mwanadamu hawezi kukipangua.

No comments:

Post a Comment