Saturday, April 06, 2013

UWOYA..NITAKUSANYA VIPAJI VYA UIGIZAJI KOTE TANZANIA...WATU WA MOROGORO NA DODOMA KAENI TIYARI


Desemba 12, mwaka jana Bongo Muvi walifanya uchaguzi mkuu na kupata viongozi, viongozi hao ni Irene Uwoya ambaye aliibuka kidedea kwa kuwa Makamu Mwenyekiti huku Mwenyekiti akiwa ni Vicent Kigosi ‘Ray’.


Starehe ilimtafuta Makamu Mwenyekiti ambaye ni Irene Uwoya na kufanya naye mazungumzo lengo kubwa likiwa ni kutaka kujua ni kwa jinsi gani anaweza kuinua na kukuza vipaji vya wasanii.


Starehe: Ukiwa ni kiongozi wa Bongo Movie Group unaizungumziaje sanaa?
Uwoya: Sanaa kwangu ni zaidi ya ubunifu na ndiyo maana moja ya malengo yangu ni kubadilika na kufanya kitu tofauti kitakachovutia na kuonyeshga utofauti.


Starehe: Ni aina gani ya muvi ambazo unapenda kucheza au kushiriki?
Uwoya: Nashiriki muvi yoyote ilimradi inilipe mimi na iwe na ujumbe mzuri ambao utatoa funzo kwa jamii inayotuzunguka,hasa ukizingatia sisi ni kioo cha jamii.
Starehe: Mbona siku za hivi karibuni mmekuwa si kioo cha jamii tena badala yake mmekuwa miale mibaya kwa wanaowatazama?


Uwoya: Nakubali kwa upande mmoja na ninakataa kwa upande mwingine.
Starehe: Mmh …..mbona husomeki una maana gani kukubali na kukataa kwa pamoja!
Uwoya: Nakubali kwa kuwa baadhi yetu kweli wanakiuka maadili na ninakataa kwa kuwa jamii inataka kumbadilisha mtu kutoka alivyozoea na kumtaka aishi wanavyotaka wao kwa kuwa amekuwa msanii kitu ambacho ni kigumu.


Starehe: Sijakuelewa na ninadhani wasomaji wetu pia hawajakupata vizuri fafanua.
Uwoya:Ninachomaanisha hapa ni kwamba mavazi, kuongea na vitu vingine kama hivyo ni kila mmoja alivyozoea tangu anakuwa na ukizingatia wengi wetu tumeanza kuigiza tukiwa watu wazima, tatizo jamii inamuhukumu mtu kutokana na inavyomwona na siyo matendo yake mimi siamini kama Bongo Muvi wote wana tabia mbaya kama inavyosemwa .
Starehe: Kwa hiyo unataka kusema nini?


Uwoya: Si kwamba nawakataza watu kuwaza kile wanachowaza inawezekana kina uweli, lakini ninachotaka kusema ni kwamba mavazi siyo kigezo cha kumuhukumu mtu kinachotakiwa ni kuangalia amevaa wapi na wakati gani,


Starehe: Enhee
Uwoya: Sisi hatuonani na jamii mara kwa mara hadi kwenye shughuli maalumu na kama unavyojua sisi tumeshakuwa maalumu pia hivyo inabidi tuvae nadhifu na kulingana na eneo tulilokuwepo, hapo ndiyo tatizo linapoanzia, kwani hata aliyekuona kwa mara ya kwanza anaanza kukulaumu, jamani mbona misibani tunavaa kama watu wengine, siyo kweli kwamba muda wote tunatembea tukiwa tumevaa mavazi hayo.


Starehe: Kuhusu uhusiano usio rasmi je?
Uwoya: Hakuna uhusiano usio rasmi, kila mtu anachofanya amejipanga kukifanya, kuachana na kuwa na uhusiano mpya ni uamuzi wa mtu kitu ambacho ni ngumu kukiingilia kwa namna yoyote ile.


“Ninachoweza kusema ni kwamba sehemu za kupata wapenzi ni zile ambazo unazunguka mara nyingi, ni mara chache kupata mchumba sehemu ambayo hujawahi kufika na ndiyo maana wasanii wengi wanakuwa na uhusiano na wasanii wenzao.


Starehe: Kwa hiyo!
Uwoya:Sasa kutokana na uhusiano kuwa wa watu maarufu kwa namna moja ama nyingine ndiyo maana unakuwa gumzo, lakini kuna wasanii wanavuma kwa kuwa na uhusiano mpya hawajafikisha hata wanaume wanane au tisa ,tatizo ni kwamba habari zao zinasikika sana kwa kuwa wao ni maarufu, sikatai kama kuna kitu kibaya, lakini kuhusu uhusiano kila mmoja ana uhuru wa kuwa na rafiki ampendaye na hakuna kizuizi kuwa hata wakishindwana waendelee kuishi kwa kuwa wao ni kioo cha jamii.


Starehe: Una mpango gani wa kuibua kizazi kipya cha waigizaji ?
Uwoya: Mipango kama Bongo Muvi ipo mingi, lakini mimi ninataka kuwaibua tena wengi wa kutosha kwa kufanya ziara mikoani na kuchagua kwa utaratibu maalumu na kwa kuanza naanzia mikoa ya Morogoro na Dodoma na nitafanya hivyo kwa mikoa mingine kadri ninavyokuwa na muvie mpya.

chanzo mwanchi

No comments:

Post a Comment