Saturday, April 20, 2013

WAREMBO WAGOMBEA KUMPA NAMBA MZUNGU...

Otilia Boniface kulia na Janeth Tingisha

Wanenguaji wa Bendi ya Extra Bongo, Otilia Boniface na Janeth Tingisha mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa kali ya mwaka baada ya kutaka kutwangana makonde wakigombea kutoa namba zao za simu kwa buzi la Kizungu.

Tukio hilo lilitokea ndani ya Ukumbi wa Meeda uliopo Sinza jijini Dar ambapo awali Mzungu huyo alivutiwa na wadada hao hivyo kuwafuata na kuomba namba ya simu ya mmoja wao.

Kufuatia ombi la Mtasha huyo, kila mmoja alitaka apate nafasi hiyo ndipo wanenguaji hao waliposukumana na kufikia hatua ya Janeth kuchukua simu ya Otilia na kuipiga chini ila kwa busara za Mzungu huyo alichukua namba za wote.

No comments:

Post a Comment