Saturday, April 20, 2013

YALIYOTOKEA KWA KANUMBA,BI KIDUDE,SHARO,SAJUKI,MARIAM,MZEE KIPARA PWAGU,MLOPELO,TUMECHOKA NAYO HUU NI WAKATI WA SEREKALI KUZAMA NDANI ZAIDI

 
Nina kila sababu ya kuandika hii habari kwakuwa imekuwa kamakasumba na pengini tunataka kuifanya kama mila yetu na wakati sivyo ilivyo kwa jamii ya kitanzania au ya kiafrika kabisa,najua leo pengine ni kachukiwa na wengi kutokana na ukweli huu uliojitokeza katika uhai wa bibi yetu ambaye kwasasa ni marehemu bi kidude binti baraka.

Kwanza niwapongeze wale waliojitolea kwa udi na uvumba kumsitiri bibi yetu katika makazi yake ya milele japo mvua ilikuwa nyingi lakini hakuna aliyejali hilo wote wakiwemo maraisi wetu Jakaya kikwete na Ali shen,wasanii mbali mbali wa miliki wa vyombo vya habari waandishi na wananchi wote kwa ujumla waliohudhuria pale nakumsitiri bibi yetu,ama kwa hakika kwangu nasema inshaallah mungu atawalipa kwani hamkujali mvua mlisimama mlilowa ila mlihakikisha bibi yetu mpendwa anazikwa kwa heshima zote.

Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania Dk Jakaya na
Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi ndugu
Ali Mohamed Shein wakiwasili makaburini kwa ajili ya maziko

Pamoja na yote hayo ila kuna jambo mi nadhani halipo sawa kwani ni ukweli ulio wazi kuwa tunajua jinsi bi kidude alivyokuwa anaumwa na hata maisha yake binafsi yalivyokuwa ya kawaida kama sio ya shida tena magumu tofauti na kazi yake ilivyokuwa,mtakumbuka ilifikia hatua bibi huyu akazushiwa kifo yote hiyo ni kutokana na kuzidiwa kwake

Kwangu na muita bi kidude ni simba wa muziki wa taarabu na mwamba imara uliotikisa na kuitangaza tanzania njee ya nchi kwa kiasi kikubwa sana lakini kwa bahati mbaya kafa akiwa maskini,neno hili kafa akiwa maski ni neno ambalo linapendwa sana katika misiba ya wasanii nadhani tunakumbuka kwa mzee kipara kwa tx mosh wiliam,steven kanumba,sharo milioner,sajuki,mariamu muimbaji wa taarabu na wengine wengi waliotangulia mbele ya haki ndilo neno kubwa kwao.

Lakini kitu cha kujiuliza mbona hakuna mabadiliko kama tumeshajua kuwa wasanii ni maskini?mimi labda sijui mtanisaidia wadau sijawahi kusikia msanii wanchi kama uganda kenya moroco sauth africa,nigeria ghana au kwa wenzetu ulaya kafa alafu watu au serekali yao ikatangaza msanii huyu kafa maskini sijui labda kama nyie mmesikia,ila hapa kwetu ni jambo la kawaida kusemwa msanii flani kafa maskini.

Mwana F.A na Fid Q pi walikuwepo

Mi nadhani huu sasa ni wakati wa serekali yetu tunayoipenda kuimarisha mahusiano na wasanii na kujua wanachohitaja na kulifanyia kazi kwani tasnia ya muziki,filamu,uchongaji,mipira yote ikiwemo tenesi ni sehemu kubwa sana ya ajira duniani kote je hapa kwetu bado hatuoni hilo na kuamini kuwa inaweza kutupunguzia mzigo wa ajira kwa vijana na wazee.

Boss Ruge wa Clouds Media akiwa tapa tapa makaburini baada ya mvua kubwa kunyesha pembeni yake mwenye kanzu ni mflume wa taarabu Mzee Yusuph

Mimi nadhani bado hatujachelewa na huu ndio wakati wa serekali yetu kuamka na kuingalia upya sera ya sanaa nnchini badala ya kila siku kusimama katika misiba ya wasanii na kusema flani halingani na kazi yake amekufa akiwa maskini hii ni aibu kwa taifa letu ninaamini mikakati ipo na itatuwezesha kufika mbali.

Hebu tizama picha hapo chini jinsi watu walivyojitowa

Jana alasiri ilikuwa safari ya mwisho kwa Bi kidude baada ya kumaliza
swala na kumpumzisha
kwenye makazi yake ya milele......maelfu ya wananchi wakubwa
kwa watoto walifurika sana
kwenye mazishi ya kikongwe huyu alietutoka ghafla 17april majira
ya saa 7 mchana kwa saa za afrika
ya mashariki.....Viongozi wengi wa nchini walijumuika na familia
katika maziko ya Bi kidude pamoja hata na
wasanii pia walikuwepo kuonesha mchango wao.....

Zifuatazo ni picha wakati maiti ikiswaliwa Mskitini na safari ya kuelekea makaburini kwa maziko
Raisi wa serekali ya mapinduzi  znz akiwasili eneo la msikitini

Mwili wa marehemu Bi Kidude ukitolewa nje ya mskiti tayari kabisa kwa kuelekea
makaburini....baada ya kumaliza kuswaliwaLicha ya mvua kali lakini watu walihakikisha mpaka
 mwili uingie kaburini na tufukie ndio na
mengine yatafata....

Uinzi ulikuwpo wa kutosha
Viongozi wanchi wakiwasili makaburini tayari kabisa kwa maziko
Rais Jakya alihairisha ziara yake ya nchini Uholanzi na kurudi kuja kumzika
legendary wa Tanzania,Fatuma binti Baraka.....
Issa Michuzi nae alikuwepo kuhakikisha akosi matukio kwa ajili ya habari za mitandao

Mwana Fa  na Fid Q baada ya maziko........awakujali mvua
...kuwanyeshea ...lakini bibi aende salama..No comments:

Post a Comment