Sunday, May 19, 2013

DIAMOND ASEMA PENNY AMEKUBALIKA KWAO KILICHOBAKI NI HARUSI TU

Mwanamuziki mwenye makeke mengi na ambaye hadi sasa anaongoza kwa  kutajwa tajwa sana katika vyombo vya habari Diamond platnumz ameongea na thesuperstars na kuweka wazi kilicho moyoni mwake juu ya mpenzi wake ambaye kwasasa ni mjamzito.

Akipiga stori na thesupestarstz msanii huyo ameeleza wazi kuwa anampenda sana mchumba wake na amemuandalia zawadi kubwa sana mara atakapojifungua salama,msanii huyo ameendelea kueleza kuwa kwasasa anamuomba mungu amjalie mchumba wake ajifungue salama ili waanze maisha mapya ya kumlea mtoto wao.

Thesuperstars tz ilitaka kujua kama maneno ya dada yake diamond yana ukweli ndani yake kwani ni hivi karibuni dada wa msanii huyo alikaririwa akisema kuwa kaka yake yupo kwenye maandalizi ya ndoa bila kueleza ni siku gani ndowa hiyo  itafanyika

Kwa upande wa diamad alisema kuwa dada yake hawezi kudanganya jambo hilo ni la kweli na akasisitiza kuwa kwasasa asingependa kuliongelea sana kwani lina muda wake na muda ukifika mambo yote yatakuwa wazi kwa kila mtu huku akisisitiza kuwa muda si mrefu atamuoa penny kwani ndio chaguo lake

Penny kwa sasa nikama mke wa diamond kwani wapo pamoja  na mara nyingi sana penny anapatikana sinza mori nyumban kwa msanii huyo huku mama yake diamond akisema amemridhia penny kuwa na mwanae na atafurahi sana siku mwanae akimuoa mwanadada penny kwani ndie mwanamke pekee aliyeweza kuwa na madili ya mke na anaamini watadumu na mwanae kwani ni dhahiri wmependana.

Diamond kwasasa anamalizia nyumba yake maeneo ya tegeta ambayo anasema nyumba hiyo iliyogharimu milion mia mbili sitini ni zawadi kwa mama yake mzazi kwa malezi bora hadi kufika hapo alipo  huku  nae akiwa katika maandalizi ya ujenzi wa nyumba yake na penny.

Baada ya kumaliza ziara yake ya kimuziki nchini uingereza diamond sasa anajipanga kwa ziara ndefu nchini sweden na denmark,Kwasasa maneja wangu yupo katika maandalizi ya show zangu nyingine nchini sweden na denmark na itakuwa ziara ya mwez mzima kisha nitarudi bongo alisema msanii huyo mwenye kuongoza kwa kufanya show nyingi ndani na nnje ya nchi kwa garama kubwa.

Tulipata bahati ya kuongea na mwadada penny na kumuliza mawili matatu ambapo hakuwa na mengi ya kusema bali kumuomba mungu ajifungue salama na kusisitiza anampenda sana mchumba wake huyo na anaamini mungu atawasaidia na watakuwa mume na mke kwani wote wanapendana sana tofauti na inavyofikiriwa alisema mwanadada huyo ambaye ni mtangazaji wa tv.
No comments:

Post a Comment