Thursday, May 30, 2013

HII NDIO TAARIFA YA JOHN MAGUFULI KUHUSU KUGOMBEA URAIS 2015

Siku chache baada ya waziri wa Africa masharik Samuel sitta kumhusisha waziri wa ujenzi John Magufuli kugombea urais 2015,Waziri huyo ameibuka na kupinga kauli hiyo kwa kusema kua hakuwahi kufikiria kitu kama hicho.

   Waziri wa Africa mashariki alinukuliwa akiwataja mawaziri wenzake ambao wata gombea kiti hicho cha urais ni yeye Samuel sitta,Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Bernad Membe,Waziri wa uchukuzi Dr,harrison mwakyembe ambapo sitta alisema watachagua mmoja kati ya hao ambaye atagombania urais mwaka 2015.Alisema hayo juzi kwenye kongamano katika nyanja za digitali kwa wanafunzi wa mawasiliano wa st augustino{SAUTI}

     Alisema hato gombea tena ubunge baada ya kua katika ulingo kwa miaka 35 na ataangalia namnanyingine ya kuwatumikia wana nchi na ndipo alipo gusia suala la uraisi na kusema anamuachia mungu alisema SAMUEL SITTA

      Kauli ya waziri wa ujenzi John magufuli akiwa nje ya jengo la bunge dodoma alisema kua hana mpango wakugombea urais na hajui lolote kuhusu mchakato wa urais na haelewi kauli ya waziri mwenzake huyo.

      Magufuli alisisitizia kua hana kundi na hajawahi kuhudhuria kikao cha kundi lolote na hatarajii kua na kundi lolote.Ninachojua kundilangu ni CCM na mwenyekiti wake ni jakaya kikwete.

       JE KATIKA LISTI ILIYO TAJWA HAPO JUU YA WAGOMBEA URAIS UNADHANI YUPI ANAWEZA KUICHUKUA NCHI KAMA AKIPEWA NAFASI???
         TUANDIKIE COMMENT ZAKO HAPA CHINI KWA YEYOTE ULIYE SOMA HII POST NA KUIELEWA

No comments:

Post a Comment