Wednesday, May 01, 2013

MASTAA WA BONGO WALIOVISHWA PETE ZA UCHUMBA NDOA ZIMEISHIA NDOTONIWema Sepetu akiwa na pete aliyovishwa na Dimaond.


KATIKA ulimwengu huu kuna mambo mengi yanayofurahisha. Yapo pia yanayosikitisha na utapeli katika uhusiano wa kimapenzi umetamalaki.

Nimeanza na utangulizi huo nikiwa na maana kuwa katika jamii inayotuzunguka inabidi mtu uwe makini lasivyo utajikuta kwenye wakati mgumu hasa kwa wasichana wanaohitaji kuolewa.Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume kuwarubuni wanawake wakiwadanganya kuwa watawaoa, ahadi ambazo hazitimii…

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanaume kuwarubuni wanawake wakiwadanganya kuwa watawaoa, ahadi ambazo hazitimii kwani mapenzi yao huwa yanaishia njiani kabla hawajatimiza lengo na kuwaacha wenzao katika maumivu makali.
FLORA FESTO MVUNGI
Ni mwigizaji wa filamu za Kibongo anayeishi kinyumba na mwanamuzki wa Kizazi Kipya, Hamis Ramadhan Baba ‘H. Baba’.
Tangu Flora avishwe pete ya uchumba na H. Baba pamoja na kutolewa mahari, siku zimesonga bila kuona suala la ndoa likiendelea.
Wasanii hawa kila wakiulizwa kuhusu suala la ndoa huwa wanajibu hivi karibuni ambapo kwa sasa kuna madai kuwa tayari Flora ana ‘kibendi’.


ROSE DONATUS NDAUKA
Ni staa mkubwa wa filamu za Kibongo ambaye alichumbiwa kwa muda mrefu na jamaa aliyekuwa mmoja wa kundi la kitambo la Bongo Fleva kutoka Tanga la TNG, Malick Bandawe.
Rose amekuwa akiahidi kila kukicha kuwa harusi yake iko mbioni lakini umepita muda mrefu hakuna ndoa wala nini na badala yake wamebaki kuishi pamoja kama mume na mke.OTILIA BONIFACE
Ni mkata mayenu kiraka wa Bendi ya Extra Bongo ‘Wazee wa Kizigo Staili’. Alivishwa pete ya uchumba miaka miwili iliyopita na mume wa mtu anayejulikana kwa jina moja la Ally lakini mpaka sasa ndoa imebaki ndotoni.
Otilia na mchumba wake huyo wanaishi pamoja kama mume na mke na suala la ndoa bado wanajiandaa.SUZAN CHUBWA ‘QUEEN SUZY’
Ni mnenguaji bei mbaya wa Bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’. Alivishwa pete ya uchumba zaidi ya miaka miwili iliyopita na aliyekuwa rapa wa bendi hiyo, Aimerichard Mwamba ‘G-Seven’ ambaye kwa sasa amehamishia makazi yake Nairobi, Kenya na kumwacha Suzy Bongo. 
G-Seven alimposa Suzy pamoja na kumvisha pete ambapo uchumba wao ulidumu kwa muda mrefu kabla ya hivi karibuni bishosti huyo kuweka wazi kuwa ameamua kuachana naye kwa sababu aligundua kuwa siyo mwaminifu.ISABELA MPANDA
Ni Miss Ruvuma 2006. Anasaka mkate wa siku kupitia filamu na muziki wa Bongo Fleva. Alivishwa pete ya uchumba kitambo na kutolewa mahari na mwanaume jina kapuni lakini aliishia kupewa mimba na kuzaa.
Baada ya kuzaa Isabela mpaka sasa hajaolewa na amejaliwa kuwa na watoto wawili kila mmoja na baba yake huku ikifahamika kuwa yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanamuziki Luteni Kalama.MIRIAMU GERALD
Ni Miss Tanzania 2009 aliyevishwa pete ya uchumba na msanii wa filamu za Kibongo, Kennedy Victor ‘Kenny’. Walipanga kufunga pingu za maisha mwezi Juni, mwaka jana lakini hadi unaposoma hapa hakuna chochote zaidi kujaliwa mtoto mmoja wa kiume.WEMA SEPETU
Ni mwanadada mrembo kutoka kiwanda cha filamu za Kibongo. alivishwa pete ya uchumba na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ lakini mapenzi yao hayakufika mbali, waliishia kuachana na mambo ya ndoa yakaishia hapo huku bidada akiendelea kujikusanyia pete za uchumba kabatini kwake baada ya ile ya Yusuf Jumbe.SHAMSA FORD
Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye kwa muda mrefu amechumbiwa na jamaa mmoja aitwaye Dick. Uchumba wao una zaidi ya miaka miwili lakini ndoa imekuwa ni kitendawili huku wakijaliwa mtoto mmoja wa kiume aitwaye Terry.SALMA JABU ‘NISHA’

Ni staa wa filamu za Kibongo ambaye aliwahi kudaiwa kuvishwa pete ya uchumba na mwigizaji mwenzake aitwaye Godfrey Kusila kabla ya uchumba kuvunjika na penzi kuhamia kwa mwanamuziki Elibariki Emmanuel ‘Ney wa Mitego’. Hata hivyo, kwa Ney wa Mitego napo uchumba uliota mbawa pamoja na kuwa na mbwembwe nyingi.

1 comment:

  1. hii blog inaongoza kwa kuiba habari za blog zingine, oya kuwa mbunifu na siyo copy and paste bila hata kubadilisha habari kidogo wala kuweka link za unaowaibia habari zao. tuko mbioni kuweka hadharani bloggers wote kama wewe, kama hujui kazi waachie creative bloggers wanaojua kutafuta habari mtutukera mpaka cc wasomaji.

    ReplyDelete