 |
Hapa Dude akimkimbiza mama yake hosptalini bila kujua kwamba mama yake kashafariki dunia. |
Kulwa
Kikumba, msanii wa maigizo aliye maarufu kwa jina la Dude, amepata pigo
kubwa baada ya kufiwa na mama yake mzazi asubuhi ya leo jijini Dar es
salaam. Katika ujumbe wake ambao ameutuma kwa wadau wake, msanii huyo ameandika
"Ndugu zangu wapendwa, nimefiwa na mamaangu mzazi niliyempenda kuliko
mtu yeyote kwenye dunia hii, leo saa 12 asubuhi. Inna Lillah waa inna
illah rajiun"
(Pichani ni msanii huyo akiwa kwenye gari akimpeleka
mama yake hospitalini kwa matibabu, kumbe mama huyu tayari alishakuwa
ameiaga dunia"
Binafsi na wadau wa thesuperstarstz kwa ujumla, tunampa pole Dude kwa pigo hili na tuna ahidi kuwa pamoja nae kwakila hali
Mungu ampe
nguvu ya kuweza kusimama imara katika wakati huu mgumu kwake na familia
yake kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment