Wednesday, May 01, 2013

MTOTO WA CHUCHU HANSI NI MOTO WA KUOTEA MBALI KATIKA FILAMU,CHEK BUDY,RAY,JOHARI,WAMNGANGANIA ..MA DIRECTOR WAUMIZA VICHWA KUPATA STORI INAYOMUHUSU ILI WAMCHEZESHE

Farihiya katika pozi
Farihiya akiwa katika scen na chek budy

Kwa hakika waswahili husema mtoto wa nyoka ni nyoka na simba hawezi kuzaa swala hili limejidhihirisha wazi kwa mtoto Farihiya  mwenye kipaji cha ajabu na anakuja kukimbiza vilivyo katika soko la filamu tanzaniag

Mtoto huyu ambaye ni mtoto wa kwanza wa msanii wa filamu nchini chuchu hansi ameonyesha kumrithi na pengine kuja kumzidi  mama yake mzazi kwa jinsi alivyoonyesha umakini na uchezaji wa hali ya juu katika filamu hiyo ya Rj.

Hapa akiwa na wasanii wenzake kama johari chek budy na crew ya Rj akipokea maelekezo toka kwa Director
Farihiya mtoto mwenye kipaji cha ajabu ameshirikiana na wasanii wakubwa katika kazi hiyo kama Blandina chagula johari,Mohamedy Nurdini Cheki Budy,Stanlay Msungu Senetor,Mzee Masinde,na wengine wengi,wakipiga stori na thesuperstarstz wasanii hao kwa nyakati tofauti wamemuelezea mtoto huyo kuwa ni moto wa kuotea mbali na kuwaasa wasanii watoto kukaa mkao wakula kwani mtoto huyu ni balaa.

Hapa Farihiya katika scen na Chek budy wa pemben aliyeshika bumu ni sound man wa kutegemewa Rj
Mimi ni produser wa filamu na nimefanya filamu nyingi za kuwashirikisha watoto ila mtoto huyu ana kipaji cha ajabu kwanza ushikaji wa script wa farihiya ni balaa pili uchezaji tatu anakijua kingereza vizuri si chakubabaisha hii itamsaidia kuwa msanii wa kimataifa zaidi tofauti na wenzake wanatumia kiswahili tu na kujikuta wanalizunguka zaidi soko la ndani alisema chek budy.

Kwa upande wa johari alisema kampuni yake haibahatishi kwani humlenga mtu kulingana na story pili  hata ubora wa picha zetu tumeongoza na tumechukua tuzo nyingi sana za kampuni yenye kutengeneza filamu bora zenye muonekano mzuri kuanzia picha sauti na mwanga.hivyo nachoweza kusema anakuja kwa kasi na ameonyesha makubwa katika filamu hii ya wrong hope alisema johari

Hapa aki show love na Camera man profesional wa Rj company
kwa  uapande wa  yeye alipohojiwa na thesupestarstz alisema anamshukuru mungu kumpa kipaji hicho na ameahidi kukitumikia mara atakapo maliza shule,Unajua kkwasasa nipo shule so nikimaliza shule nitaingia rasmi katika soko la filamu ila nategemea kusomea kabisa filamu ili nichanganye na kipaji alisema 
Sifa yake kubwa hapendi kupoteza muda akimaliza scen anauliza kama anashuti kisha huingi kusoma  screpti
Kwa upande wa chuchu ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo alisema kwanza kwake ni faraja kuona amepata rafiki na mtu pekee anayeweza kurithi kipaji chake na anafurahishwa sana na hilo ndio maana anajitaidi kumpa suppot kwa kila kitu anachokitaka kukamilisha ndoto yake,Kusema kweli nafurahi sana kwani nimepata mtu wa kunirithi kipaji changu nitajitadi sana kumpatia malezi bora na kumuonyesha njia pekee za uigizaji ili afikie malengo yake ikiwa ni pamoja na elimu ya kutosha,aliendelea kueleza mama huyo wa watoto wawili.

Hapa akiwa na make up wa Rj
 Ama kwa hakika mtoto huyu ameanza vyema kwani thesuperstarstz imezisikia kauli kadha za mastar ambao pia ni ma director wakiongea kumtafutia filamu kali ili acheze,kwa upande wa farihiya mwenyewe alipoulizwa kama annaipenda sanaa alisema naipenda sana ila kwa sasa sitaki tena hadi nimalize shule naipenda shule sana aipohojiwa kama ikitokea akaitwa tena atakuwa tayari aliji kwa kifupi nitakuwa tayari bt iwe haingiliani na shule kama ilivyokuwa hii
Hapa akiwa na Mr creator Steven shoo lightman Director
 Nae Director wa movie hiyo Juma Chikoka au Chopa amesema mara nyingi filamu zinazosumbua katika kuziongoza huwa ni za watoto ila amekiri kuwa katika filamu hii hajapata tabu kwani huyu mtoto amekuwa kama msanii mkubwa kwanza anashika script na anacheza katika kiwango cha juu sana hadi mtu unashangaa

Hapa akiwa na Said Baraghash sound man wa Rj
 Ama kwa hakika Farihiya anaonyesha kuja juu hivyo wadau mpeni suppot kwani mama yake tu hawezi bila nyinyi wadau thesuperstarstz imeshuhudia filamu hiyo ikirekodiwa maaeneo ya mbezi huku produser wa movie hiyo blandina chagula johari akiongea na thesuperstarstz nakusema kuwa  huu ni muendelezo wa projrct ya kampuni yake kudili na movie za watoto toka Rj na lengo likiwa ni kuinua vipaji vichanga ili kukuza sanaa yetu ya tanzania kimataifa zaidi alisema johari.ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Rj company

No comments:

Post a Comment